Wanaokosoa ubora wa Simba na wanaosifia wote wana hoja, wasikilizwe

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Mimi kwangu naona pande zote mbili wana hoja, kuna wanaokosoa uwezo wa timu na kuna wanaosifia.

Wanaokosoa wanaona Simba haichezi vzr ingawa inashinda, wanajua Simba inavyocheza, Simba wanatandaza sana soka ya chini, mpira unapigwa had unaomba refa aongeze muda usiishe, wanaona timu haichezi kwa kuvutia, hawajaanza kuiona Simba ikicheza Leo wala jana, hawa wanajua Simba inavocheza, wao kushinda sio hoja isipokuwa tunashindaje, yaani chemistry haipo, upangaji wa kikosi sio mzuri, wachezaji wazuri hawapewi nafasi na wana uwezo, kuna wengine wametumikia kwa muda mrefu hawapumzishwi, dimba la kati haliwajibiki, wanaamini Simba ingeweza kumaliza mchezo kule kule Zambia, wanaona ule uchezaji wa Yanga ndio hasa uchezaji wa Simba u

Livyo.Hawa wana hoja, wanaongea kwa mapenzi na Simba, wasionekane maadui, wanataka kuiona Simba ikifika mbali, mbona nyie mnaosifia hamtukanwi, mbona watu hawasemi mnatafuta ulaji ndani ya uongozi, Robertinho abadilike, ni kocha mzuri tunaheshimu taaluma yake lakini kiwango hakipo kiviiiile.

Tusitukanane, kila mtu ana haki ya kutoa maoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…