Wanaokutwa na fumanizi la SHILAWADU 'wanajitakia' na wanalipia kipindi

kilambimkwidu

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2017
Posts
6,097
Reaction score
7,199
Wakuu,

Nilikua na adabu mjini nikiwa maeneo yangu nikijua kwamba labda nitadakwa na kamera za Shilawadu lakini kumbe "hakuna shilawadu wanaofumania"

Ukiangalia jinsi wanavofanya vipundi vyao (mazingira na maandalizi ya mhojiwaji) shilawadu ni kama hua wanavizia 'mastaa' wakiwa kwenye pozi mbovu na kuanza kuwamulika na kamera za shilawadu. Lakini sasa imefahamika (pasi na chembe ya shaka) kwamba hawa wambea hua hawavizii kama wanavojinasibu, ispokua wanakutana na 'star' kabla na kupanga fumanizi liendaje kabla hawajamfumania.

Leo wamemwaga ubuyu wa msanii mfupi Sheta na Sheta anajifanya hataki kuhojiwa kwakua wamemshitukiza lakini ni hivo juzi tu Sudy alikua na Sheta pale MarkJuice Sinza na Sheta alikua akipiga domo anabembeleza "afumaniwe"
 
we unaonaje mkuu? wanalipa au wanajitakia?
 
we unaonaje mkuu? wanalipa au wanajitakia?
Tukimpata Sheta atathibitisha hilo...atatuambia arrangement ilikuaje kwa upande wake. Ila ninachosema ni kwamba juzi nlmwona na Shilawadu wakiyajenga
 
Mmh sina uhakika. We taarifa hizo umezipata wapi mkuu
 
kuna siku walikuwa wanamfuatilia bambo, wakajisahau wakamuonyesha bambo akiwa na mic yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…