Wanaokwenda kwa waganga wana hoja, wasibezwe

Wanaokwenda kwa waganga wana hoja, wasibezwe

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
5,718
Reaction score
7,784
Jumatano njema!

Kuna ubaya kusema kila mtu anakula anakopeleka mboga? Wapo WaRC na Walokole wengi hukimbilia kwa waganga wa kienyeji na miilini wana chale za kutosha.

Wana hoja, miaka ya leo utapeli umekuwa mwingi. Mchungaji anafukuza muumini kwa uzinifu wakati mwenyewe anazini.

Watu wamedanganywa mno na wamechoka kudanganywa. Inaonekana wengi siku hizi wanaponea kwa waganga na si makanisani.

Injili ya kina Paulo iko wapi?

Wachungaji na manabii mjitathmini sana kwa yanayotokea kwa kondoo wenu. Hii siyo dalili nzuri.
 
Tumetoka kwenye ushoga naoona sasa waganga nao wameshika hatamu, haipiti siku bila kuona uzi kuhusu uganga.
 
Mchungaji sijui nabii ni mlozi tu nae katoka Nigeria kuchukua uchawi aje akuloge usijielewe. Halafu anakuhubiria habari njema ili umpe sadaka na mali zako.

Mtapata lini akili?
 
Mchungaji sijui nabii ni mlozi tu nae katoka Nigeria kuchukua uchawi aje akuloge usijielewe. Halafu anakuhubiria habari njema ili umpe sadaka na mali zako.

Mtapata lini akili?
Kaka inatia uchungu sana hasa kwa hawa Manabii wengi uchwara. Wao wana magari ila waumini wao wengi ni choka mbaya hatari. Kmmk napata hasira
 
Back
Top Bottom