Wanaolala sana kushikwa na Kiharusi

Wanaolala sana kushikwa na Kiharusi

Mr.Black

Member
Joined
Jun 9, 2014
Posts
97
Reaction score
74
Watu wanaolala kwa zaidi ya masaa manane kwa siku wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa kiharusi,utafiti umesema lakini wataalam hawajua sababu yake.Utafiti uliofanywa kwa takriban watu 10,000 katika chuo kikuu cha Cambridge ulibaini kwamba wale wanaolala kwa takriban saa nane wana uwezekano mkubwa wa asilimia 46 kupata kiharusi.
Watu wazima hupendelea kulala kati ya saa sita na tisa ili kupumzika vizuri,lakini kulala zaidi hushirikishwa na matatizo ya afya kama vile ugonjwa wa sukari pamoja na ule wa kunenepa kupitia kiasi.
Hatahivyo haijabainika kutoka kwa utafiti huo iwapo kulala kwa zaidi ya saa nane huenda ndiko kunakosababisha matatizo hayo ambayo husababisha kiharusi ama iwapo ni miongoni mwa sababu za magonjwa yasiojulikana.
Utafiti huo ulifanywa miongoni mwa watu walioko na kati ya miaka 42 na 81.

Watafiti walichunguza mienendo yao ya kulala kwa kipindi cha miaka 10 ambapo watu 346 walipatwa na kiharusi.
Baada ya kuangazia athari kama vile miaka na jinsia, watu waliosema wamekuwa wakilala kwa zaidi ya masaa manane walipatikana na hatari ya asilimia 46 kupatwa na ugonjwa huo.
Wale walioweza kulala kwa chini ya masaa sita walipatikana na hatari ya asilimia 18. SOURCE NI BBCSWAHILI.COM
 
Na kulala chini ya masaa sita ni kujitafutia msongo wa mawazo kutokufikiri vizuri uwezekano wa kupata ajali ukiendesha sababu ya uchovu stress nk
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Bora kulala sana kuliko kutokulala kabisa.....WALALAJI WENZANGU SAANA MUPOOO????
 
Napiga usingizi TBC ukweli na uhakika hadi najiogopa daaa nikiamka saaafiii nakuwa stable and fresh sasa hizi habar kwa kweli zimenisikitisha
 
Back
Top Bottom