Wanaomaliza vifungo waonywa kutojihusisha na uhalifu

Wanaomaliza vifungo waonywa kutojihusisha na uhalifu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini, amewaonya wafungwa na mahabusu wote nchini kuacha tabia ya kujihusisha na uhalifu pindi wanapomaliza kutumikia vifungo vyao na kuachiwa huru jambo linalopelekea kurudi gerezani kwa mara nyingine.
42483619-9b66-4308-b2f1-806aaf965ae9.jpeg
Ametoa Onyo hilo alipotembelea na kuzungumza na wafungwa pamoja na mahabusu katika Gereza la Bangwe lililopo Wilaya ya Kigoma ambapo aliongozana na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, na kuwataka wawe na maadili mema pindi watokapo vifungoni.

Amesema baadhi yao wamekuwa wakirudi gerezani kwa mara nyingine kutokana na matukio ya kihalifu waliyokuwa wakiyafanya baada ya kurudi uraiani.
577f7e7f-afea-4b5a-8ee6-e0d94705baf9.jpeg

07ffe4ef-26c7-452d-aa58-ac3f30c8eee6.jpeg
Amewataka wawe mabalozi wazuri kuhamasisha jamii kuwa na maadili mema, utii wa sheria na kushirikiana Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika kuzuia uhalifu.

“Ndugu za niwaombe pindi mnapomaliza kutumikia vifungo vyenu na kuachiwa huru muache tabia ya kujihusisha tena na magenge ya kihalifu jambo linalopelekea baadhi yenu kurudi gerezani kwa mara nyingine na badala yake mkawe mabalozi wazuri mkahamasisha jamii kuwa na maadili mema, utii wa sheria na kushirikiana Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika kuzuia uhalifu”. Alisema Mhe. Sagini
 
Back
Top Bottom