Wanaomiliki silaha kinyume wazisalimishe kwa hiyari

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Desemba 4, mwaka jana, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, aliagiza kwamba mtu yeyote au kikundi kinachomiliki silaha kinyume cha sheria wazisalimishe kwa hiyari ndani ya siku 30.

Dk. Nchimbi alisema kuwa baada ya muda huo kupita, vyombo vya dola vitafanya msako wa kuzitafuta silaha ambazo wamiliki wake watakuwa wamekaidi kuzisalimisha wenyewe kwa hiyari.

Dk. Nchimbi alielekeza kwamba silaha hizo zisalimishwe katika vituo vya polisi, wenyeviti wa vitongoji, vijiji, watendaji wa kata, taasisi za kidini wakuu wa wilaya na mikoa.

Hatua hiyo inafuatia kuzagaa na matumizi holela ya silaha hizo, ambazo zimekuwa chimbuko la matukio ya kasi ya uhalifu nchini, unaohusisha matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Dk. Nchimbi alisema kuwa kumbukumbu zilizopo na taarifa za operesheni zilizofanyika maeneo mbalimbali nchini kuanzia Januari hadi Septemba, mwaka juzi, zinaonyesha kuwapo kwa matukio 876 ya uhalifu, ukiwamo unyang’anyi wa kutumia silaha.

Katika kipindi hicho, silaha 62 ziliibwa ama kunyang’anywa kutoka kwa wamiliki wake halali na jumla ya silaha 304 zilikamatwa katika matukio mbalimbali ya uhalifu.

Takwimu zinaonyesha pia kuwa katika kipindi hicho, matukio ya ujambazi yalikuwa 876, ambayo yalisababisha vifo 138 vya raia na askari polisi sita.

Aidha, katika kipindi hicho, jumla ya mali zenye thamani zaidi ya Sh. bilioni 4.5 ziliibwa kwa kutumia silaha zinazomilikiwa kinyume cha sheria, zikiwamo zinazomilikiwa kisheria, lakini zinatumika isivyo halali.

Alisema kuwa takwimu hizo zinaonyesha kwamba, miongoni mwa jamii kuna watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria na isivyo halali.

Kufuatia agizo hilo la Waziri Nchimbi, baadhi ya wamiliki wa silaha hizo wameitikia na hadi kufikia Jumatatu ya wiki hii, jumla ya silaha 310 zimesalimishwa kwa hiyari.

Wizara ya Mambo ya Ndani imesema kuwa tangu agizo la Waziri kutolewa, silaha nyingi zimekuwa zikisalimishwa serikalini kutoka kwa watu mbalimbali na hakuna hatua zozote walizochukuliwa wahusika kwa kuwa wamezisalimisha wenyewe. Pamoja na kwamba baadhi wamezisalimisha silaha hizo wenyewe, lakini tunaamini kuwa silaha nyingi bado zinamilikiwa na watu kinyume cha sheria na zinaendelea kutumika katika matukio ya uhalifu.

Silaha hizo bila shaka ndizo zinazotumika katika kufanya vitendo vya uhalifu hususani wa unyang’anyi kama takwimu za mwaka juzi zinavyobainisha.

Matukio ya matumizi ya silaha kwa mwaka 2012 yalikuwa mengi, jambo linalodhihirisha kuwa watu wengi wanamiliki silaha kinyume cha sheria kiasi kwamba hata katika matukio ya uhalifu mdogo zinatumika silaha nzito kama bunduki au bastola.

Kuzagaa kwa silaha kumewarahisishia wahalifu kuua, kujeruhi na kuwapora raia mali zao. Kwa mfano, kumekuwapo na kasi kubwa ya wahalifu kuteka magari katika maeneo mengi ya nchi na kuwapora wasafiri fedha na mali nyingine. Baada ya muda uliotolewa na Waziri Nchimbi wa kuzisalimisha silaha hizo kwa hiyari kesho, vyombo vya dola havinabudi kufanya msako wa nguvu nchi nzima ili kuzikamata silaha zote ambazo zinamilikiwa kinyume cha sheria.

Kwa kuzikamata silaha hizo na wamiliki wake waliokaidi kuzisalimisha, hatua hiyo tunaamini kuwa itasaidia sana kupunguza kiwango cha matukio ya uhalifu nchini kuanzia mwaka huu.

Zoezi la kuwataka wamiliki wa silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha linapaswa kuwa endelevu na lifanyike kila mara sambamba na operesheni ya vyombo vya dola ya kuzisaka kwa watu ambao wanazimiliki kinyume cha sheria.

Mtu anayemiliki silaha kinyume cha sheria maana yake ni kwamba aliipata kwa lengo la kuitumia kufanyia uhalifu na siyo vinginevyo.

Raia wana wajibu mkubwa wa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Jeshi la Polisi ili kufanikisha ukamataji wa silaha halamu pamoja na wamiliki wake kwa njia ya kutoa taarifa.

Polisi peke yao hawawezi kufanikisha jukumu hili peke yao bila kutegemea taarifa za raia ambao wana taarifa sahihi za wahalifu kwa kuwa wanaishi nao. Kila mtu akitimiza wajibu wake kwa kutoa taarifa sahihi, bila shaka matukio ya ujambazi yatapungua.



CHANZO: NIPASHE

 
Ok, maneno mengi - hata hivyo hoja yako nini. Manake ninachokisoma ni maneno 'Nchimbi akasema....' yakijirudia tuuuuuuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…