Wanaomlaumu Julio na timu yetu ya vijana U 20

Wanaomlaumu Julio na timu yetu ya vijana U 20

MAKULUGA

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2011
Posts
7,828
Reaction score
10,527
Timu yetu ya vijana U 20 imerudi mikono mitupu kutoka Mauritania baada ya vipigo viwili na sare moja.

Kama kawaida wapenda soka waneiponda vibsya timu yetu. Ila wengi wamemlaumu kocha Julio na kuhitimisha kuwa Hana uwezo!

Kwa mpenda soka mkweli na mfuatiliaji lawama kwa Julio ni za ajabu.

Kumbuka tumefungwa na Ghana na Morocco ambazo zimewekeza mno mno kwenye soka. Unapoongelea soka la vijana nchini Ghana unaongelea kiwango Cha Dunia. Hivi unataka uwafunge Ghana kirahisi hivo kwa lipi.

Hivohivo Morocco wapo mbali mno! Sisi saizi yeti no Wale tuliotoka nao droo.

Watanzania tusipende njia ya mkato kwenye mafanikio.

Itakuwa ni kutomtendea haki Mungu na Waghana waliotumia akili ktk kuendeleza soka, ukiwafunga kirahisi. Kuna nyakati mafanikio hupita njia ya bahati, tuombe hilo litokee lakini ktk hali ya kawaida, bado Sana! Tusimbebeshe mzigo Julio!

Leo mafanikio ya Simba tunayo yaona hayajashuka Kama Mana kuna kitu kimefanyika!

Kwa wano mlaumu Julio eti kwa Nini tumefungwa na Ghana na Morocco, wote ni Utopolo wakubwa!
 
Hatumlaumu Julio kwa sababu ya uwekezaji, Julio hana mbinu. Mi hizo mechi sijaziangalia, ila mechi ya mwisho ya maandalizi tuliocheza hapa Chamazi na Uganda , nakumbuka ile mechi tuliwafunga Uganda, kuna jamaa tulikua naye tunaangalia ile mechi, nikamwambia hatuvuki hata makundi. Sio kwa sababu hatuna vipaji ila hatuna kocha.

Julio nafikiri alikua anawambia tuna ingia na 4:3:3 basi amemaliza. Timu inacheza kama vile wanacheza cha Ndimu, huoni basic za uzuiaji hata moja kila mmoja anajirudia tu nyuma kukaba, hajui arudi kukaba katika shape gani, hiyo ni kazi ya kocha sio uwekezaji, Labda tuwalaumu TFF kwa kutokumpa timu kocha mwenye mbinu za kisasa.

Mpira saizi umebadilika mno, unachezwa kisayansi mno. Julio bado anafundisha kizamani mno. Julio pale ni msimamizi wa mazoezi, tunavipaji hatuna makocha wanaoendana na sayansi ya mpira.

NB: Kuna timu ipo buguruni kuna brother anajiita kocha anawafundisha vijana pale, asilimia kubwa ni watoto wanaotakiwa kukuzwa katika mpira.

Yule sio kocha ni msimamizi wa mazoezi, maana hakuna hata siku moja kwa muda niliyokua naenda kuwaangalia niliona anawafundisha style of playing.

Akishafanya mazoezi ya viungo anawagawa anawaambia wacheze. Amemaliza.

Niliwaza nikasema inawezekana hii hali ipo kwenye vituo vingi vinavyojiita vituo vya kukuzia vipaji. Wengi ni wasimamizi wa mazoezi sio makocha
 
Back
Top Bottom