#COVID19 Wanaopinga Chanjo za Uviko-19 wasipingwe bila kutafakariwa, wanaopigia debe wasiungwe mkono bila kuhojiwa

#COVID19 Wanaopinga Chanjo za Uviko-19 wasipingwe bila kutafakariwa, wanaopigia debe wasiungwe mkono bila kuhojiwa

Joined
Jul 22, 2021
Posts
7
Reaction score
5
Na Nkuruma wa Karne ya 21.;[emoji3578]

Oooh Chanjo hii inafaa Sana, Ni muhimu Sana, ooh ni hiari kuvhanjwa, ooh hapana Chanjo iwe lazima, jamani haifai inamadhara; kauli lukuki zinapita katika masikio ya watanzania, Waafrika na Wanadam wote kote duniani.

Kukosoa ama kupigia debe Chanjo hizi si kosa na kila anayechagua upande wa kuamini Hana kosa kwa mujibu wa Sheria za Tanzania na Sheria za Kimataifa kwani ibara ya 18 na 19 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamini katika uamzi na misimamo binafsi ya mtu na hivyo kutoa Uhuru na haki ya mtu kuamini na kusema ama kusimamia anachokiamini bila kubughuziwa kwa kulazimishwa kuamini imani ama mawazo ya mwingine, ndivyo ilivyo katika mikataba mbalimbali ya Kimataifa ikiwemo ule wa Mikataba wa Kimataifa wa haki za kisiasa na kijamii yaani, International Covenant on Civil and Political Rights (ICCPR) katika ibara mbalimbali.

Changamoto hapa Ni je hawa wanaopinga Chanjo hizi Ni wao? na kama Ni wao wanapinga kwa hoja zipi na kwa maslahi ya Nani? Nao wanaounga MKONO Chanjo hizi, je Ni wao? Wanaunga mkono kwa hoja zipi na kwa maslahi ya Nani? Mbona wanatumia nguvu (lobbying) kubwa kulamisha watu kuziamini?

Mataifa ya 'Magharibi' yalikuwa ya Kwanza kuathiriwa na Uviko 19, tahadhari takachukua na sisi Afrika na Tanzania tukapitiwa na janga hili na hakika tahadhari tukaiga na tukaendelea na maisha.

Baadaye mataifa hayo ya magharibi yakaja na Chanjo, muda mfupi baada ya Chanjo madhara ya Chanjo yakaanza kuibuka na sitifahamu ikaendelea huku Chanjo zikizidi kubadilika majina na kuongezeka lakini zote zikitoka huko, kila Muafrika aliyetangaza Kinga ama tiba ya Janga hili alibezwa Sana na Waafrika wenyewe kwa nguvu shinikizi kutoka kwa mataifa haya ya magharibi.

Swali kwa mtu Mwenye akili timamu; je wazungu ndio wanastahili kugundua tu na si waafrika? Je wazungu wanampango wa Siri wanaoujua kuhusu Uviko 19 na Chanjo hizi? Je Ni Janga tu nao kweli wanashangaa Kama sisi na Chanjo Ni Kinga halali na yenye lengo jema hata wao walioigundua ndiyo wanayochanjana Ni hii hii na Wala Haina madhara yale yanayozushwa?

Kinachozua tafakuri zaidi ni kuwa, Wakati Janga hili linaingia nchini na juhudi Kali kuanza kuchukuliwa ikiwemo kuanzisha vituo vya kuhifadhi wasafiri wanaotoka nje ya nchi na wale wanaoonekana kuwa karibu na mtu anayekutwa na maambhzi ya Uviko 19 kwa Siku kumi na nne wakiwa wametengwa, Mamlaka zilitangaza kupuuzwa kwa ugonjwa huu na kuamuru maeneo yaliyokuwa yakiwahifadhi watu hao kuwaruhusu kutawanyika Mara moja, urainani waliingia na tukakaa tuone matokeo huku hotuba za viongozi zikitawaliwa na matumaini, ibada na kupuuza taarifa za Uvico 19 na kwa nguvu zote Chanjo za Kinga zilippingwa hadharani

Baadaye, kufuatia kifo Cha aliyekuwa Rais wa serikali hiyo ya awamu ya tano, Hayati John Magufuli, taarifa za Janga la Uvico 19 zilianza kutangazwa, kwa nguvu masharti ya kujikinga yakarudi, Chanjo zilizopigwa zikaansa kupigiwa debe na Sasa ndio uhalisia unaoendelea katika jamii.

Hayo yote Ni sawa lakini kinachozua taharuki ya kifikra kwa wenye ubongo usio na kutu, waliohuru dhidi ya makundi ya kiitikadi na ufuasi wa watu Ni kuwa; Walewale walioipinga Chanjo kuwa Ina madhara na kusisitiza tiba mbadala Leo ndio wanaoipigia debe Chanjo hiyo kuwa inafaa sana, Wale waliohitaji Chanjo na takwimu za Chanjo kutolewa leo baadhi yao wanalalamika kuletwa Chanjo hizi, Mataifa ya 'Magharibi' yanatumia nguvu kubwa kushawishi watu waiamini Chanjo, wachanjwe, yanatumia zawadi ya pesa za mikopo kwa nchi zikitoa takwimu za maambukizi na kupokea Chanjo, na Sasa yanadaiwa kutangaza kuwalipa fedha taslimu wale watakaochanjwa (Marekani ikiwemo).

Tunao wanajamii wasomi, vijana kwa wazee, wanasiasa na wanataaluma mbalimbali ; aliyepuuza kuzungumziwa Uviko 19 walimshangilia kuwa huyo alikuwa mtu makini sana na wakasimama naye, aliyepiga marufuku Chanjo hizi walimpigia makofi na Wakamsaidia kuandaa ajenda za kuchafua sifa ya Chanjo hizi, Ni Walewale aliyerudisha utolewaji wa taarifa za Uviko-19 wanamshangilia Sana na kumwona mtu makini sana, Ni Walewale Leo wanapigia debe Chanjo hizi na kumwona anayechanjwa Ni mtu makini sana.

Ni watu hawahawa, Mheshimiwa Rais wa awam ya tano, Hayati Magufuli alipokataa Chanjo walimpigia makofi, Rais Samia alipotangaza Chanjo ije na iwe hiari wakapiga makofi, Askofu aliposema Chanjo haifai wakamshambulia, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe aliposema iwe lazima wakamshambulia, najiuliza leo Rais Samia akisema Chanjo iwe lazima watatamka kipi!

Hapa ndipo Panafanya kujiuliza Hawa wanaopinga Chanjo hizi Ni wao? Ama kunanini nyuma yao na kwa maslahi ya Nani? Wanakijua wanachikipinga? Na wanaounga mkono Chanjo hizi je Ni wao? Wako huru ki maamzi? Ama nini kimejificha na kwa maslahi ya Nani? Wanakijua wanachikipigia debe?

Askofu Gwajima, alitumia hoja nzito kuikosoa Chanjo ya Uviko 19 lakini waliomkosoa wengi bila kujali elimuna nyadhifa zao hawakuzivaa hoja zake dhidi ya Chanjo Bali walimsakama yeye na ufu wake yaani hoja zake zilibaki imara akashambuliwa yeye elimu yake, kazi yake na maisha yake kwa ujumla (Attacking personality instead of the arguments raised).

Kwa hoja hizi chache na mwenendo mzima wa Janga hili na jinsi linavyokabiliwa duniani kote, wanaohoji na kukataa baadhi ya Chanjo si wajinga Bali wasikilizwe hoja zao na wajengwe kwa hoja Bora zaidi ya zile za kwao na wale wanaounga mkono Chanjo hizi si wajinga Bali wasiungwe mkono bila kuhojiwa na wao kutetea Chanjo hizi kwa hoja.

Busara ya kibinadam; wale wanaopinga Chanjo na tiba hizi, je wagonjwa ambao tayali wapo na tatizo hili tunawaweka katika tiba zipi? Na wale wabaotaka Chanjo iwe hiari na mtu ajaze form, je watoto wadogo na wanafunzi huko mashuleni na makundi maalumu wengine haki yao ya kuamua na kusimamia maamzi inalindwa na Nani na kwa utaratibu upi? na Hawa wanaowatukana wale wanaosema Chanjo Zina madhara, je ikitokea siku za usoni ikathibitika Chanjo hizi kuwa Zina madhara kwa waliochanjwa tutaambizana Nini?

Tunifunze kuheshimu fikra za watu, tusikubakiane bila kuhijiana na Wala tusibezane bila kutafakariana, hoja zivunjwe kwa hoja na kushambulia utu wa mtoa hoja. Je wewe unaamini lipi Ni sahihi katika mwenendo wa Janga hili na hatua zinazichukuliwa na dunia?

Tukiwa huru kifikra, tukasimama na kweli kadiri ya fikra zetu na imani zetu duniani Ni mahali salama Sana kuishi.
 
Wewe umesimamia upande up? Je unahisi upo huru kuamua
 
Back
Top Bottom