Wanaopinga Katiba Mpya wapo makundi matatu

Wanaopinga Katiba Mpya wapo makundi matatu

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2021
Posts
3,085
Reaction score
4,890
Suala la kudai Katiba Mpya ni la lazima kwa sababu kuna makundi 3 yanajitahidi sana kupinga isipatikane.

Makundi hayo ni
Kuna kundi lisilo na Uwelewa wa katiba iliyopo na katiba mpya

Kuna kundi la wastaafu kwenye Chama cha CCM na Serikali hawa ni wanufaika na katiba iliyopo kwa uhalali au sio halali kwa mali walizonazo.

Kuna kundi la waliopo madarakani kwa katiba iliyopo kundi hili linakula keki ya taifa
makundi haya ndio wapinzani wa katiba mpya.

Makundi haya ndiyo wanatoa vijisababu visivyo na tija eti tunajenga uchumi
Tanzania imekuwa na uchumi mbovu kwa miaka 60 kutokana na katiba iliyopo leo utajenga uchumi kwa katiba iliyoshindwa kujenga uchumi kwa miaka 60?

Watanzania kama tunataka maendeleo tunatakiwa tudai katiba mpya.

Viongozi Waliopo madarakani na wabunge wanakula keki ya taifa na familia zao.

Hawana uchungu na umasikini wetu ndio Maana masikini tunapitishiwa Masheria ya Hivyo ya kodi na wabunge
 
katiba mpya sio takwa la kisiasa. ni takwa la kitaifa.

ila ajabu wanaoitaka ni chadema peke yao, wanaoikataa ni ccm peke yao.

wananchi wanaendelea na maisha mengine.
 
Hoja ya katiba haina mashiko kwa sasa, dunia nzima ipo fcd up kwa taharuki ya corona, uchumi wa dunia na nchi mbalimbali umeyumba, mipango mingi ya kiuchumi imevurugika, katikati ya hali hii nyie mnadai katiba!! Inaweza kuwa dai sahihi, lakini si kwa muda huu! Katiba can wait, kuna mambo mengi yanahitaji immediate actions kuliko hiyo katiba
 
Ukiwauliza michadema kwamba kwanini unataka katiba mpya?

Yatakwambia ni ili tupate urahisi wa kwenda ikulu.

Kwa hiyo katiba inadaiwa na mijitu itakayojinufaisha kisiasa. Na huu ni upumbavu kama upumbavu mwingine tu
 
CCM Mjengoni aka MILO MITATU aka Tumechukuwa tumeweka Waa, hawaitaki katiba ya Warioba kwa kuwa hawana uhakika wa kurudi mjengoni au kuendesha/kutawala nchi wapendavyo hivyo wanawarubuni CCM Mkunguni aka Wanyonge kuwa katiba mpya italeta machafuko na itavunja muungano.

CCM Kurishishana ndio hao wenye dira ya Chama Chao au kampuni yao ya kuitawala nchi kisultani miaka elfu.Hawako tiyari kuona CCM kuachia madaraka kwa kuwa wataumbuka.Kwa undani ni kama secret society,wana ushawishi mkubwa kwa umma,wana fedha na mali,wana nguvu katika vyombo vya ulinzi na usalama.Kwa lugha nyepesi wao ndio wenye nchi.
Hata Raisi SSH akitaka mabadiriko ya katiba hatafurukuta kwani huko nyuma Raisi Kikwete alianzisha mchakato wa Rasimu ya Warioba akaishia njiani.
Hata enzi ya Raisi Mwinyi bunge la Chama kimmoja kilipitisha muswaada wa serikali 3 ukiongozwa na G55,lakini cha kushangaza akatokea mtu asiye Raisi wa JMT au Mwenyekiti wa CCM,akaikataa,katishia kujiondoa kwenye chama kama muswaada hautafutwa.Na kweli muswaada ulifutwa,Waziri Mkuu na Katibu Mkuu wa CCM walifutwa kazi,na akawatungia kitabu.
 
Back
Top Bottom