Nitaipinga hoja yako mkuu kupitia kipengele chako cha mada chenye maneno "Historia ya maungamo ya dhambi katika agano la kale"
Nianze kwa kukupa history kidogo. Mara baada ya anguko la Adamu na Hawa pale Eden Mungu alikuwa ameshaanda mpango wa wokovu wa Mwanadamu ndiyo maana utaona kuna mnyama alichinjwa pale ili wapate nguo za kuficha uchi wao lkn halikuwa lengo hasa Ila alichinjwa ili awe mbadala wao kwa dhambi walizotenda ndiyo maana hawakufa kama sheria isemavyo ya mshahara wa dhambi ni mauti.
Kutokea hapo utaona ibada za kafara kupitia wanyama zikianza kwa kila aliyekuwa akitenda dhambi na hata habari ya ukuhani pia baadaye hema ya kukutania ilipoanzishwa katika kitabu cha kutoka 25 agizo la ujenzi wa hema hiyo lilipotolewa.
Katika ujenzi ule Mungu anamwambia musa kuwa hema ile itakuwa mfano wa ile ya mbinguni kwa hiyo note hata mbinguni kuna huduma ya upatanisho kupitia kuhani
Turudi kwa mada hema ya kukutania Ilikuwa na sehemu kuu tatu uwa wa nje, patakatifu na patakatifu pa patakatifu ambapo ktk uwa wa nje ndiyo sadaka za kuteketezwa zilipotolewa ambapo mdhambi alitwaa kondoo kama mbadala wake na kwenda naye kwa kuhani ambaye aliact kama mpatanishi baina ya mwanadamu mdhambi na Mungu ambapo aliungama dhambi zake kwa kuweka mikono yake juu ya kichwa cha kondoo kama namna ya kuhamisha dhambi kutoka kwake kwenda kwa kondoo kisha alimchinja na kuhani kukinga damu na kuingia nayo kwenye chumba cha pili cha patakatifu kwa ajili ya kufanya upatanisho wakati kondoo akiteketezwa katika ua wa nje huu ndiyo ulikuwa utaratibu wa wokovu ulioandaliwa na Mungu kabla ya Kristo kuja duniani
Baada ya Kristo na kufa kama mwanakondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu yohana 1:29 na kufa pale msalabani habari za kwenda kuungama kwa kuhani zilikoma au huduma za kikuhani na utoaji kafara ulikwisha maana huduma ile ilikuwa kivuli kumuwakilisha Kristo na sasa Kristo ameshakuja hakuna haja tena kwenda kwa mwanadamu kuungama wakati Kristo yupo
Kwa hiyo hoja yako ya kuungama kwa padri ni kutaka kuturudisha kwa huduma ya kikuhani ya mwanadamu ambayo ni hatari sana maana unapinga kwamba Kristo bado hajafa kwa ajili ya dhambi na wewe unageuka kuwa mpinga Kristo
Leo hatuna haja ya kuungama kwa mwanadamu tena maana tunaye Kristo mwombezi wetu kuhani asiyepatikana na mauti anayehudumu ktk hekalu lisilofanywa kwa mikono ya mwanadamu huyo pekee astahili kutuombea msamaha kwa Mungu Baba na si mwingine yoyote