Mahakama ya Kadhi
Mheshimiwa Mufti;
Kuhusu mchakato wa kuanzisha Mahakama ya Kadhi, nimeyasikia maoni yenu kwamba kumekuwa na kulegalega kwa upande wa Serikali jambo linalowafanya muingiwe na wasiwasi kuhusu nia njema ya Serikali katika mchakato huu. Napenda kuwatoa hofu kuwa hakuna kulegalega wala kubadilika kwa dhamira ya Serikali. Msimamo wa Serikali upo pale pale. Huu ni uamuzi uliofanywa na Chama chetu na Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya uongozi wa Rais Benjamin Mkapa wa kutaka kulitafutia ufumbuzi suala la Mahakama ya Kadhi na kuachiwa Serikali ya Awamu ya Nne kutekeleza.
Na sisi katika kufuatilia utekelezaji wa jambo hili tulikabidhi Tume ya Kurekebisha Sheria kuishauri Serikali. Ushauri wa Tume hiyo ulikuwa kwamba Serikali haiwezi kuunda Mahakama ya kushughulikia masuala ya kidini ya dini fulani. Jambo hilo liachiwe Waislamu wenyewe kufanya.
Serikali imekubali ushauri huo na ndipo mchakato ukaanza na tukaunda Kamati ya pamoja iliyojumuisha Serikali na BAKWATA. Nia ya Serikali ni kujihakikishia kuwa hicho kitakachoundwa hakiendi nje ya masuala ya kidini yaani ndoa, takala, mirathi na wakfu kwa mujibu wa dini ya Kiislamu. Katu si Mahakama ya kushughulikia masuala ya jinai au madai. Haitajihusisha na masuala ya wizi na kutoa adhabu kama vile za kukatwa mikono. Haitahusika na kesi za fumanizi na hivyo kutoa hukumu ya kuuawa mkosaji kwa kupigwa mawe. La hasha !! Narudia kuwa mamlaka yake yatahusu ndoa, takala, mirathi na wakfu. Isitoshe Muislamu hatazuiliwa kuamua kutumia sheria za nchi kwa masuala hayo akipenda kufanya hivyo.
Mheshimiwa Mufti, Waheshimiwa Masheikh, Ndugu Zangu Waislamu;
Napenda kuwatoa hofu pia kwamba hakuna mkono wa mtu wapo mnadhania hivyo. Maana, tunajuana. Si ajabu kuna hisia kuwa huenda Kanisa limeingilia kati kuzuia au kuchelewesha. Siyo hivyo hata kidogo. Tarehe 22 Julai, 2011 nilipoalikwa kuzungumza na Maaskofu katika kikao chao cha Jukwaa la Wakristo katika risala yao kwangu kuhusu suala la Mahakama ya Kadhi walitoa ushauri ufuatao kuwa:
"Kuanzisha Mahakama ya Kadhi nchini na jambo zuri linalowahusu Waislamu. Kwa kuwa ni jambo la kidini waachiwe Waislamu wenyewe walifanye ndani ya Uislamu, pasipo kutumia hazina ya Serikali ambayo ni fedha ya walipa kodi wote nchini"
Hiyo ni nukuu kutoka ibara ya 6 ya Risala yao kuhusu Uhuru wa Kuabudu na dhana ya Udini.
Katika maelezo yangu kwao, niliwahakikishia kuwa mawazo yao yanawiana na yale ya Serikali kama ilivyoshauriwa na Tume ya Kurekebisha Sheria ambayo Mwenyekiti wake ni Profesa Ibrahim Juma. Mahakama hii itaundwa na Waislamu wenyewe ndani ya Uislamu wao na wataiendesha wenyewe na haitagharamiwa na Serikali.
JK
Assume wewe ni muislam na una wake watatu na watoto 5:4:3 yaani 12 jumla kwa wake watatu..umefariki
Kwa sheria za ndoa ya 1971; ugawaji wa urithi huo hauwezekani japo muislam huyu aliruhusiwa kuoa kiislam
Kwanini mali yake isigawanywe kiislam?? tunataka kadhi wawasaidie hao wanawake, watoto kuhusu mgawanyiko wa mali ya muumini huyu.. siyo voluntarily iwe sheria kabisa na hukumu itolewe na mahakama..ok
Ndio maana tunataka mahakama ya Kadhi..
NB: Naomba wale wenye hasira na uislam na waislamu watuache kwanza tuseme kwanini tunataka mahakama ya kadhi ili mtuelewe
Mkuu, JK sii Mungu wala Katiba.. tunachofuata ni katiba inasema nini na maadam katiba inatambua sheria za asili kwa nini wasiwe na mahakama inayojali na kutafsiri sheria hizo. Sheria ya nchi itambue ndoa ya wake wanne lakini matatizo ya ndoa hizo yaamuliwe kienyeji wakati sheria zipo? -Ndivyo unavyotaka kusema!Ingawa hili si jukwaa la dini lakini kwani kuna mtu amewazuia kuanzisha mahakama yenu labda hukumwelewa rais soma hapa
We Topical, kama umemsoma Feedback na hujaridhika ukate rufaa, sio kuleta upya mijadala iliyokwishatolewa ufafanuzi wa kina kwa wenye uelewa: Hakuna aliyepinga kuanziswa kwa mahakama yenu, anzisheni kulingana na taratibu za dini yenu.
Msitake kila kitu kuanzishiwa na serikali kwa kodi za wananchi.
Pili kama ulivyosema kuwa suala hili ungependa mjadili ninyi waislamu tu, ni ruksa ila mngeweza kufanya hivyo zaidi msikitini badala ya kuleta hapa JF
Kama kweli unataka so called "Intellectual Arguments" basi ungeweka hii mada kwenye jukwaa la sheria ili watu wajadili kisheria sheria na kikatiba katiba. Zaidi ya hapo itakuwa n ihisia na ushasbiki wa kidini. ukichanganywa na siasa.
Mimi comment yangu moja tu kwenye uzi niulize wachangaji wote watakapenda kuchangia na mleta mada
je wewe kama ungekuwa mwanasheria mkuu wa serikali uko tayari kurushu na kumshauri raisi akubali kuingiza rasmi mfumo wa mahakama za mila za wajaruo, wahaya, na makabila mengine kwenye mahakama ya JMT.
NB
Agalizo kuna mila zina utaratibu wao mfano wa mirathi
ni makosa kulinganisha wahaya na uislam ok..
Nimeuliza tatizo lenu nini hasa?
Kama ni fedha serikali inalipa mahakimu sasa kwa kuendesha kesi za waislamu ambazo wanakosea sana hukumu
Kwa hiyo kukiwa kadhi hela hiyo hiyo inayotumika sasa ndio itatumika ok
usiwe na wasiwasi na hela ok..
naomba solution ya mambo haya niloyaeleza hapo juu..
Mtoa mada unachekesha kweli yaani mahakama ya kadhi kwa ajili ya ndoa sita saba kumi.....? kwani wewe unapoa zaidi ya mke mmoja tayari ni tatizo kwa nini usijiandae mapema kabla mungu hajafanya maamuzi yake na mahakama ya Jamhuri ya Muungano itawatendea haki uliowaacha nyuma. Jaribu kufanya research kwa nchi zote ambazo zina mahakama ya kadhi kama hao wajane au watoto walipata haki yao baada ya baba/mume kufariki? Next??????!!!!
Assume wewe ni muislam na una wake watatu na watoto 5:4:3 yaani 12 jumla kwa wake watatu..umefariki
Kwa sheria za ndoa ya 1971; ugawaji wa urithi huo hauwezekani japo muislam huyu aliruhusiwa kuoa kiislam
Kwanini mali yake isigawanywe kiislam?? tunataka kadhi wawasaidie hao wanawake, watoto kuhusu mgawanyiko wa mali ya muumini huyu.. siyo voluntarily iwe sheria kabisa na hukumu itolewe na mahakama..ok
Ndio maana tunataka mahakama ya Kadhi..
NB: Naomba wale wenye hasira na uislam na waislamu watuache kwanza tuseme kwanini tunataka mahakama ya kadhi ili mtuelewe
ni makosa kulinganisha wahaya na uislam ok..
Kama ndoa mliifunga kwa imani ya dini fulani, na kwa imani hiyo mnataka kugawana urithi tatizo lipo wapi kutumia taratibu za dini hiyo mpk mpelekane mahakamani? Ukiona mtu hataki utaratibu wa dini ktk kugawana mirathi basi ina maana haitaki na dini yenyewe. Huu ni utaratibu wa kulazimishana kufanya mambo kwa nguvu.
Mbona ndoa hamfungii mahakamani?