Wanaopinga mahakama Kadhi "Intellectual Arguments" only

Status
Not open for further replies.

Hakuna swala la kuassume hapa,ni ukweli ulio wazi katika ndoa ya Kiislam wake ni wengi ni ruksa kisheria.

mahakama za serikali na mirathi hizo hua ni halali,tatizo ni kukosekana mfumo maalum ambao umeamliwa ka QURAN yao kuhusu Kadhi,bado kama waislam wanayo namna ya kuanzisha kufuata taratibu zao kama zilivyoamliwa na kitabu chao.
Lakini kwa namna ambaywaislam wamesimama kutaka mahakama za kadhi zianzishwe sambamba na mahakama zingine kisheria,lazima kuna ajenda nyingine iliyojificha nyuma ya madai hayo. Sioni sababu ya Waislam kushindwa kuanzisha hizo mahakama ndani ya UISLAM wao wakiwa na haki ya kikatiba ya UHURU WAO WA KUABUDU huku wakiendelea kulalamika na kutaka kuanzisha fujo wakati jambo lenyewe lipo ndani ya uwezo wao kisheria.

Labda nikuulize wewe uliye uliza swali, wake zako wote ni WAISLAM,Ndugu zako waislam,hata watoto pia,NINI KINAWAPELEKA MAHAKAMA za kawaida kugawa mirathi na mshindwe kutumia taasisi zenu za kidini kugawa mirathi hiyo ?ambapo ugawaji ungezikatia maamrisho ya Quran yenu ?

Sheria ya ndoa hiyo ya 1971 inatambua uwepo wa NDOA ya Kiislam,sasa kama sheria hiyo inatambua uwepo wa ndoa hiyo maana yake inatambua hata namna ya ugawaji wa mirathi Kiislam,japo inajua pia kuwa huwezi kumshurutisha mtu kutumia sheria za Kiislam kama hataki.


 
Katiba inaruhusu uhuru wa kuabudu na uhuru wa mawazo...lakini kumbuka uhuru huo kama haki nyingine za kikatiba sio absolute.Unaweza kunyang‘anywa kwa maslahi ya uma,amani,utulivu nk.

Lakini pia serikali yetu haina dini yani we are a secular state..
Kwa hivo kwa mujibu wa sheria zetu serikali iko sahihi kabisa.

Pia ni Kwa sababu,kwa mujibu wa katiba yetu ibara ya 107A,chombo pekee cha kutoa haki ni mahakama.Hivyo haki kwa misingi ya dini ya kiislam inatolewa ndani ya mfumo huu huu tulio nao wa mahakama bila kuwa na mahakama ya kadhi.

Pia kwa mujibu wa Magistrates Courts Act,Masuala yote ya madai yanayogusa imani ya dini ya kiislam na mila mara nyingi huanzia mahakama ya mwanzo na kwenda mpaka mahakama za juu kwa njia ya rufaa,na bado haki hutolewa kwa misingi ya sheria za kiislam endapo wahusika wanaamini katika dini hiyo na endapo ni sahihi kwa sheria za dini hiyo kutumika kwa wahusika hao.

Lakini suala ni je, endapo waislam wanataka mahakama nje ya mfumo uliopo uhuru huo unapatikanaje sasa?Ina maana waislamu hawana uhuru wa kuanzisha mahakama kwa mujibu wa imani ya dini zao? Kwa sababu naamini mahakama ya kadhi iko ndani ya misingi ya dini yao.

Jibu ni kwamba wanaweza.Na wala serikali haijawakatalia kwa sababu ni haki yao japo sio absolute.Isipokuwa serikali haitaki kujihusisha moja kwa moja inataka waanzishe nje ya mfumo uliopo na iwe independent of the governmentt.

Hii inatokana na ukweli kwamba kimsingi serikali haina dini kwa mujibu wa katiba, na kujishirikisha katika mchakato mzima wa uanzishwaji wa mahakama ya kadhi ni kuingilia uhuru wa waislamu na pia uhuru wa wakristo kwani ni sawa na kuimpose imani hiyo kwa wakristo.

Kwa hiyo sioni vibaya waislamu kuanzisha mahakama hiyo bila kulazimisha serikali kuhusika kwani itaamsha hisia za imani nyingine kutaka serikali kujihusisha na imani zao na hivyo kupelekea chaos na kuhatarisha usalama wa taifa na stability.

Pia serikali imeruhusu kuanzishwa mahakama hiyo nje ya mfumo uliopo wa mahakama na waislamu wenyewe as long as inagusa masuala ya kadhaa tu
 
"jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza"
Mr.Ebbo R.I.P .Aliimba 'Acha kubisha bisha kitu usichokijua oyaaa........"Ukisoma historia makabila yalikuwepo kabla ya hizo dini...Huku afrika tulitofautiana kwa makabila na mila zetu na tulikua tukifanya ibada zetu za kiimani kwa wazee wetu waliotutangulia..Matatizo yaliletwa na waarabu na wazungu.waraabu na dini yao ndio walionyesha kiwango kikubwa cha udhalilishaji wa utu wa mwanadamu,kwa kutuuza kama watumwa,tena tulikuwa tunafungwa minyororo kama mbwa...Halafu ndio unataka kujifanya unamjua Mungu zaidi kuliko wengine.Sisi wapagani nani atasimamia maslahi yetu?Achaneni na mambo yenu ya dini za kuletewa ambazo waliozileta wenyewe siku hizi zinawashinda.Tunatakiwa tuishi kama watanzania tulio huru,bila kuchanganya interest za madini yenu yasiyokuwa na faida kwa wengine.Naungana na member aliesema Dini unaweza badili lakini si kabila..Hili ni kweli kwasababu kabila zimetokana na uzao,au koo ambazo zinatufanya tufanane kwa uasilia wetu,sio hizi dini tunazofundishwa historia, ya nani alifanya nini,na ukizifuatilia unapata hata shaka kama Mungu wanaemzungumzia yupo.Dini ni mambo ya kufikirika tu,ila Utanzania,utanganyika au uzanzibar ndio asili yetu na ndio kitu halisia kilichopo.Hebu tutoleeni mambo yenu ya udini wengine yanatuchafua sana.Kwani unapozaa watoto wengi kama panya huwa hamfikiri namna bora zaidi ya kuwaendeleza kimaisha zaidi ya hiyo mirathi?wapelekeni shule ndio ukombozi kuliko kitu chochote,maana mali waweza kunyang'anywa lakini vichwa vyao wataweza kwenda navyo popote pale.Tuliisha toka kwenye Ujima msitake kuturudisha tena huko.Urithi wafundisheni wadini wenu wawe wanaandika wosia kabla ya kufa.Sie wengine baba zetu walikua maskini na walipokufa walituachia vibanda vya kujihifadhi ,kila mtu amehangaika kivyake mwisho wa siku mkirudi nyumbani kusalimia ,mnarudi kwenye kile kibanda na hakina mwenyewe.Yupo mama mzazi tu.Hapo baadae mnakaa kama watu wazima kuona tuboreshe vipi.Viongozi wenyewe wa dini ambao ndio wanafundisha hayo maadili ndio watenda maovu wakubwa,halafu leo unajifanya unaijua dini kuliko alioileta.Yaani ni sawa na "kujifanya Mkatoliki kuliko pope"
Nasepa zangu mie...
 
Si uandike wosia unaofuata hiyo sheria ya kiislamu?
 
If that is serious part of your belief and prayers...muanzishe hiyo mahakama sooner than later. Na mfanye bila kupiga matarumbeta maana ni suala la dini hilo sio kampeni za kisiasa.
 

Acheni ujinga kutaneni msikitini au kokote anzisheni mahakama yenu nani kawakataza?Au kuna nini mnachokitaka mpaka muundiwe na Serikali ya watanzania?Fikra mgando hizo.Na wakristu,wapagani,kila kabila nao waombe za kwao itakuwaje?Je nchi itakalika kweli?
Upuuuuuuuuuuzi mtupu.Weka pembeni misimamo yako ya udini na uliangalie kwa akili zinazofanya kazi sawia utapata jibu hata ukiwa muislamu.
 

Sawa mkuu nimekupata kumbe waIslam Tanzania ni 35% !.

sasa si ndio maana inabidi tuoe wake wengi tuzaliane zaidi,halafu tutafute namna ya kuendesha serikali?matokeo yake unashindwa hata kuwalea vizuri watoto wako wanaanza kutegemea mirathi.Wakati wengine tunajitahidi kupunguza idadi ya watoto ilimradi kile kidogo kinachopatikana kiweze kututosheleza,nacho pia kwa maisha ya sasa hakitutoshi.sasa hapo ndo nashindwa kuwaelewa kabisa hawa jamaa.
 

Nyie mbomba hii ishu imeshatolewa maelezo? kwamba anzisheni hizo mahakama au mnalingine? Inawezeana hamko tayari ndiyo maana hamuelewi somo, hii ishu ishatoka serikalini anzisheni tu? haya mambo yanawezekana bila kutegemea mtu yeyote, mbona mko hivyo!!!!!! Kikwete na serikali yake walishajivua lawama, nyie mngeanzisha hiyo mahakama, mapungufu yatakapotokea ndiyo muombe serikali kama ina namna ya kuwasaidia lakini sasa hamtaki kuelewa. Karne hii sio ya kutegemea kusaidiwa tuuu, Pili kwa maelezo ya dini yenu vitu haramu ni marufuku, sasa kama mjuavyo serikali ya Uingereza ndiyo kinara wa kutoa fedha kwa ajili ya Tanzania na serikali hiyo ndiyo inayoitaka serikali yetu iunge mkono vitendo vya kishoga hamuoni kuwa kwa kuchangamana na serikali hizi za kiafrika kuna siku mtapokea fedha "HARAM"?

Inawezekana Kabisa kunakutokushirikiana kwenye jambo hili kati ya waislam, nyie kuweni kitu kimoja muanzishe, au mnawasiwasi mahakama hizo zitakosa wateja? maana kuna kila dalili mama akikimbilia Kwa Kadhi baba anatia timu Kisutu "Naisubiria hiyo Komedi"
 
Mi nangoja maandamano ya tarehe 23 dec.
Tena muende magogoni mkamtoe yule jamaa mumpeleke Kidongo chekundu, mumlazimishe awape haki zenu.

Msipofanya hivyo, basi nyie ni watu wa maneno mengi na lawama.

Nitakuja kuwakumbusha hapa tarehe 23 dec.
 
@Anold, kabla hata ya pesa za Cameroun ukumbuke kwamba Tbl ni walipa kodi wakubwa wa serikali, sasa je waislamu wako tayari mahakama ya kadhi iendeshwe kwa pesa za walevi wa pombe?
 

MK kwani hizo sheria za mirathi za Kiislam haziwezi kuingizwa ktk sheria za nchi na kutafsiriwa na Mahakama za Kawaida? Tatizo ni Mahakama hizo kuwa na Makafir?
 
Assume wewe ni muislam na una wake watatu na watoto 5:4:3 yaani 12 jumla kwa wake watatu.i
Ukiishi kwa sheria unaweza ukawa unafanya mambo ya ajabu sana duniani.
Ukiweka sheria mbele na busara/hekima nyuma, matokeo yake ndo haya.........

kama yupo mwanamke wa kiislamu amabye anaweza kuja hapa jamvini na kusema ukweli wake kwamba yeye kwa imani yake, hana problem kuolewa mke wa tatu au wa kwanza na mumuwe aongeze wengine wawili nbasi na afanye hivyo sasa hivi.
 
Hii dini inauchafu mwingi! hakika ukiona wanawake wanavyoteseka huko Pakistan, Afghanistani utawahurumia.
 
Hii dini inauchafu mwingi! hakika ukiona wanawake wanavyoteseka huko Pakistan, Afghanistani utawahurumia.
"Jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza"
Jamani hiyo ya 10. ni kitu gani?maana sie wengine viingereza vyetu ni vya serikalini.
 

Naunga mkono, Mahakama ya kadhi iwepo na ianzishwe na waislam wenyewe.
Mahakama hiyo iende sambamba na kuanzishwa kwa mfumo wa "Sharia" asilimia mia moja- Fully fledged Sharia law, ambayo itatumika tu kwa waislam watakao ridhia.
Bila kuwepo na Sharia law, siungi mkono kuanzishwa kwa mahakama hiyo.
Hi ni kwa sababu Mahakama hiyo haitambui watoto wa nje, na nina uhakika kuwa wapo vijana wa kiislam "wanaopiga" huko na huko kama "charger" ya kobe, wanazaa/watazaa nje halafu watoto hao wasiwe na haki kwenye Kadhi courts. Kwa hiyo kama kadhi courts inaanzishwa, iende sambamba na sharia law ambayo itawashughulikia wazinzi na waasherati ili kuzuia watoto wa nje.
Mwisho kabisa taratibu zote hizo za kuanzisha kadhi courts na sharia law, zifanywe na kugharamiwa na waislam wanaotaka/ridhia.
 
Mimi ninachoshangaa ni kwamba ...wanasema BAKWATA ni chombo cha serikali na hawakitambui kwa sababu kilianshishwa na kinawakilisha maslahi ya serikali lakini tunapokuja kwenye mahakama ya Kadhi wanasema tena ianzishwe na serikali na kuwekwa kwenye katiba/sheria za nchi...! Hapa nadhani kuna kitu kibaya kimejificha nyuma ya pazia.
 
Nimeipenda hiyo ...'Fully fledged Sharia law'...! Hii naomba ije mapema ila isimamiwe na wenyewe siyo na serikali. Sisi tutakuwa watazamazi tu wa jinsi wenzetu wanavyojicharanga mapanga ya mikono na kupopoana mawe mpaka kufa...!
 
Hivi mchakato unaoendelea wa kuanzisha mahakama ya Kadhi(mtakayo isimamia wenyewe) ambao kwa mara ya kwanza uliwakutanisha Kikwete na mashehe ikulu umefikia wapi? hakuna habari yoyote kuhusu huu mchakato huko misikitini kwenu?
 
wanaosema BAKWATA ni chombo cha serikali ni wao wao, wanaotaka mahakama ya kadhi ni wao wao........
anzisheni chombo cha waislamu basi ndugu zanguni, halafu muanzie hapo......

Hamuwezi kudai hakiki-malaria sugu........unakurupuka huko ulipo unakuja kutaka haki, wenzako wanakukana.
 


Hapo na wewe unakosea.Tafakari zaidi kabla ya kujaribu kutofautisha.
Inaeleweka kuwa kwa muislam Sharia iko static habadiliki.Pia imani za dini nyingine ni hivyo hivyo jana, leo na kesho!
Mila na desturi za makabila siyo dini lakini ni taratibu za maisha.Hao waislam unaowasemea cha ajabu, inapotumika "mode of life test"
hupatikana kuwa wanaishi kufuatana na mila zao zaidi ya wanavyouishi uislam.Matokeo yake hata mirathi zao hujikuta zikishughulikiwa kimila zaidi! So haileti maana sana unapojaribu kulinganisha na kutofautisha.Cha msingi, waislam wajitengenezee taratibu zao bila kuburuta wengine ndani! Mjue pia madhehabu na dini zingine nao wanazo sheria zao. Wakristo wa Roman kwa mfano wanazo sheria zao za kikatoliki za ndoa na wanaamrishwa katika ukatoliki watii sheria katoliki za ndoa. Je ni nani amewahi kulazimisha Serikali iingize sheria hizo kwenye mfumo wa serikali? Kawaulizeni wawaelewesheni ni vipi wanazitumia bila kuwalazimisheni nyie wengine zisizowahusu.
Kuhusu MoU, NADHANI HILI SOMO LIMESHASOMESHWA SANA HATA NA MH.Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ni muislam. Iweje yeye analielewa na kuwaelimisha na bado hamuelewi? Sitaki kuamini kuwa waelewa na wasomi wa kiislam hawaoni mantiki! Mliambiwa nanyi weke miundombinu yenu na huduma kisha muingie MoU. Hamafanyi hivyo, badala yake mnatafuta mijadala kama hii kulinganisha.Mbona havifanani?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…