Wanaopotosha maana ya Katiba, eti Watu hawali Katiba, Walaaniwe

Wanaopotosha maana ya Katiba, eti Watu hawali Katiba, Walaaniwe

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Nimesikia viongozi wengi wakiwepo wasomi wengine na PhD zao wakisema wananchi wanataka chakula wanataka maji hawataki Katiba kwa sababu hawatakula katiba. Huu ni upotishaji wa kiwango cha hali ya juu.

Katiba ni mkataba kati ya mtawala na mtawaliwa, ni jumla ya kanuni za msingi zilizoanzishwa na wananchi wenyewe ambazo zinaunda msingi wa kisheria wa sera, shirika au aina nyingine ya chombo na kwa kawaida huamua jinsi vyombo hivyo vinapaswa kuongozwa.

Sekita ya Elimu kwa mfano, inaendeshwa kwa sera na miongozo ambayo imetungiwa sheria kutokana na katiba, huwezi kujenga vituo vya Afya bila kuwa na sera bora za Afya ambazo zinatokana na katiba bora, sasa utaitenga vipi Katiba na Elimu, Afya, au Maji.

Najua wanafanya hivyo kwa maslahi binafsi kulinda vyeo nk, lkn kwa kufanya hivyo hawaitendei haki jamii isiyo na uelewa mpana wa katiba ila laana haitawaacha wote wanaopotosha.
 
Waongo sana

Kwenye Tume ya maoni ya Nyalali waliokataa vyama vingi walikuwa 80% ila wakati wa uchaguzi mwaka 1995 upinzani ulipata 39% ya kura za urais!

Bila katiba mpya kuja hatuwezi kujua kama hao ambao hawaitaki ni kweli hawaitaki.
 
Kwani hatuna katiba bwashee?
Bwa shee mwaka 1977 ulikuwa na miaka mingapi? sasa wakati huo ndiyo tuli-edit katiba ya mkoloni na kuiita Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katiba ilikuwa mahsusi ku serve muundo wa chama kimoja, waakati huo tukiita chama kushika hatamu za uongozi - tulikuwa watu tusiozidi 4 tuliyofanya hii kazi. Sasa hatuko huko tena, tuna muundo mwingine kwa hiyo katiba hii inapwaya ku serve muundo uliopo sasa.

Kwa hiyo ni hivi, Watanzania wanataka kuandika katiba yao wenyewe " katiba itakayotokana na matakwa yao, sasa kuna ubaya wowote ndugu ?
 
Watanzania wengi hatuna uelewa Nilipokuja kusikia hayo maneno na mimi nikaamini Baba wa Taifa Kusema UJINGA ni Janga la Taifa alikua sahihi kabisa na Ujinga hauishi kwa Kupata Elimu hadi PHD nimekuja kuliona hilo pia.
 
Bwa shee mwaka 1977 ulikuwa na miaka mingapi? sasa wakati huo ndiyo tuli-edit katiba ya mkoloni na kuiita Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katiba ilikuwa mahsusi ku serve muundo wa chama kimoja...
Lini na Wapi Watanzania walisema wanataka Katiba mpya?
 
Waongo sana

Kwenye Tume ya maoni ya Nyalali waliokataa vyama vingi walikuwa 80% ila wakati wa uchaguzi mwaka 1995 upinzani ulipata 39% ya kura za urais!

Bila katiba mpya kuja hatuwezi kujua kama hao ambao hawaitaki ni kweli hawaitaki.
Wangekuwa hawataki katiba mpya 2012 wasingetoa maoini kwenye tume ya Warioba
 
Back
Top Bottom