Wanaosafisha vyeti Re-Seaters

7jero

Member
Joined
Oct 8, 2021
Posts
46
Reaction score
46
Habari za majukumu wakuu,

Leo nimeulizwa swali na mdogo wangu lakini sikuweza kumjibu. Mdogo wangu alimaliza kidato cha nne miaka ya nyuma na akapata ufaulu wa div 4 point 27. Alifanikiwa kuendelea kusoma ngazi ya cheti kwa fani ya ualimu na sasa ni mwalimu wa shule ya msingi huko mkoani Shinyanga.

Amekuwa akitamani sana kujiendeleza na ndipo akaamua kuanza kusoma tuition baada ya muda wa kazi kuisha. Kwakuwa tayari alishajisajili kufanya paper mwaka huu, j3 anaanza paper lake kama private candidate.

Swali lake ni kuwa, yeye anarudia baadhi ya masomo (matatu), je ikitokea kafeli zaidi ya mwanzo cheti chake kitabadilishwa na kuwekwa matokeo haya ambayo ni latest au kitabaki na matokeo ya zamani?

Natanguliza shukrani kwani naamini kupitia hili jukwaa nitapata cha kumjibu.
 
Na tunaoresite six mnafanyaje mpaka mnafanikiwa...mi mara moja tu nilifeli na nimekata tamaa
 
Arudie masomo 7 au zaidi na Bora arudie masomo hata 9 ila target yake masomo 4au 5 tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…