Wanaosaka ' Vipaji ' vya Kukimbia mbio ndefu na fupi tukutane mijini Kesho tuvivumbue vingi tu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kila siku tunalalamika tu kwamba Tanzania haina Wakimbiaji wazuri wa Marathon ili waweze kutuwakilisha vyema katika mashindano mbalimbali huko Ulaya na hata hapa Afrika hivyo basi nina uhakika Siku ya Kesho tarehe 26 April, 2018 katika maeneo mbalimbali ya Miji nchini Tanzania tunaweza kuwapata akina Filbert Bayi na Juma Ikangaa wengi na huwezi jua hata Mrithi wa Usain Bolt kwani nina uhakika kutakuwa na mbio ndefu na fupi za ' Kutukuka ' ambazo hata Olympic hazijawahi kuwepo.

GENTAMYCINE nitakita Kambi yangu Dar es Salaam ili kuvivumbua hivyo nitaomba na Members wengine pia waliopo sehemu mbalimbali za mijini huko Mikoani nanyi Kesho mnisaidie kuvivumbua Vipaji vingine huko ili baada ya Siku ya Kesho tukaviwakilishe katika Shirikisho za Mbio za Ridhaa na Kulipwa nchini Tanzania kusudi viweze kutumika kuiletea ' Medali ' Tanzania katika mashindano makubwa yajayo.

Nawasilisha.
 
Tusiogope vitisho vyao maandamo ni haki ya kikatiba
 
Hakika kesho mbio zipo tena ni mbio hasa
 
Mwaka 2015 katika kulinda kura pale Majengo polisi moshi mida ya saba usiku,Baada kuliibua sanduku la wizi tukalipeleka kituoni na kufanya fujo mbele ya pai.Asikuambie mtu turbo niliyofungua kuelekea hostel hata Audi R8 haikuona ndani.
NB.: Uchaguzi uliisha CDM tulishinda vibaya mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…