Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Kuna Wawakilishi na Wabunge ambao wamekuwa wakitoa lugha ya kuonesha kuchoshwa na Muungano na bila ya shaka wanazo sababu ambazo wanaamini zinawapa haki ya kutoa hisia hizo. Lakini wapo wengine kati ya hao ambao wanatoa matamshi yenye kuashiria kupigania kuvunjwa kwa Muungano. Wapo wawakilishi wa vyama vyote ambao wamekuwa na kauli hizo za kutishia kuvunja Muungano hasa katika Bunge lililopita na hili la sasa. Ndugu zangu, hawa wawakilishi hawawezi kutoa kauli za kutaka kuvunja Muungano na wakabakia wawakilishi halali wa wananchi kwani kwa kutoa kauli za kuvunja Muungano wanavunja Katiba iliyowaweka hapo.
1. Wawakilishi wote hawa walisimamishwa kugombea nafasi zao au kupata nafasi zao kwa kudhaminiwa na vyama vya siasa ambavyo viliandikishwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria ya Vyama Vingi. Katiba na Sheria zinakataza kabisa kuandikishwa chama chochote ambacho kinapigania kuvunja Muungano. Hivyo, wote walisimamishwa na vyama visivyopigania kuvunjwa kwa Muungano.
2. Kutokana na hilo la kwanza, hakuna Mbunge au Mwakilishi ambaye wakati anagombea aliwaahidi wananchi kuwa ataenda kupigania kuvunja Muungano kwa sababu au kisingizio chochote kile. Wasingeweza kufanya hivyo wakati wa kampeni kwa sababu Katiba inawakataza na Sheria ya Uchaguzi ingewabana na kuwaengua mara moja. Kama hakuna chama kilichoandikishwa kwa ajili ya kuvunja Muungano hawa wawakilishi wanapata wapi mandate ya kutoa hoja za kuvunja Muungano?
3. Waliposhinda uchaguzi au kupewa ushindi wa chee waliingia Bungeni/BLW na kabla ya kuanza majukumu yao walishika misahafu na kuapa. Waliapa kwanza kabisa "kulinda, kutetea na kuihifadhi Katiba Ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania". Ninataka kuamini kuwa walimaanisha viapo vyao. Kama walimaanisha walijifunga kuulinda Muungano siyo kuuvunja. Hivyo, kauli zozote za kutishia kuvunja Muungano au hata kuashiria kuwa "muungano uvunjike" ni kinyume na kiapo chao na hivyo ni kosa tosha kabisa la kumfanya Msajili aidha kukifuta chama cha siasa au kumtangaza huyo Mbunge/Mwakilishi kuwa amepoteza sifa za kuwa mwakilishi. Huwezi kuapa kulinda Katiba halafu ukasimama kutangaza kutaka kuivunja!
4. Kama 1,2 na 3 ni kweli basi Wabunge na Wawakilishi walioko kwenye nafasi zao sasa hawana haki, uwezo, madaraka wala mamlaka ya kuzungumzia kuvunja Muungano. Yote wanayoweza kufanya ni kuutetea na kuuenzi na kuulinda.
5. Kwa vile Katiba imeweka toka mwanzo kabisa (Ibara ya 1,2) kuwa Tanzania ni nchi moja na eneo lake ni eneo lolote la Tanzania Bara na Tanzania Visiwani na kuwa katika nchi hii moja kuna vyombo viwili vya utendaji yaani Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar kauli zozote za kubadilisha serikali hizi mbili aidha kwenda serikali moja au serikali tatu nayo ni kinyume na Katiba! Wabunge hawawezi na hawapaswi kuzungumzia kubadilisha Muungano kwani Katiba Inawakataza isipokuwa kama wametekeleza utaratibu wa Katiba wa kubadili Muungano. Wameapa kulinda Nchi Moja, Serikali Mbili! Ndio maana wengine tulipuuzia na kubeza kauli ya Rais Kikwete kuwa Zanzibar ni "nchi ndani ya nchi" kwani haina mantiki na ni kinyume cha Katiba!
6. Kama 1, 2, 3, 4 na 5 ni kweli basi wabunge na wawakilishi wetu wanaachiwa uchaguzi mmoja tu nao ni kutatua kero za Muungano, kuondoa matatizo yaliyopo na kuboresha ili kuufanya Muungano uzidi kuimarika. Hawapaswi kuudhoofisha wala kutoa kauli za kuwachochea watu kuchukua msimamo wa kuuvunja. Siyo wabunge tu wale wote walioapa kulinda Katiba na hivyo kulinda Muungano wanalazimishwa na Katiba hiyo kuulinda Muungano kwa nguvu zao zote.
Hii ina maana gani?
Kwamba, kama kuna Mbunge au Mwakilishi ambaye anaona kuwa Muungano haufai na hataki uwepo anaachiwa uamuzi wa kutakiwa kutoka Bungeni (ili asibanwe na kiapo) na kwenda kuanzisha harakati za kuvunja Muungano. Na kama kundi hili linaweza kupata wafuasi basi ni jukumu lao kutumia nguvu zao zote (na hapa neno ZOTE nalimaanisha) kupigania kuvunja Muungano na kwa kufanya hivyo wajue wameamkua kupambana na vyombo vilivyopo vyenye kulinda Muungano. Kama hoja yao inaweza kuwa na nguvu sana na kupata wafuasi wanaweza kujikuta hatimaye wanalazimisha Muungano kuvunjika aidha kwa njia ya amani au kwa vurugu. Kwa vile Muungano wetu haukuwa wa ku-annex Zanzibar ni wazi unaweza kuvunjwa kwa njia ya amani kabisa. Muungano wetu siyo kama ilivyokuwa Ethiopia na Eritrea au Sudan na Sudan Kusini au Russia na Georgia au Ukraine au zilizokuwa Jamhuri za Yugoslavia. Tanganyika haikuivamia Zanzibar na kuichukua kwa nguvu. Ulikuwa ni Muungano wa Hiari ambayo kusema ukweli ni vigumu sana kuuvunja licha ya majaribio ya baadhi ya watu kujaribu kuwafanya Watanganyika wajisikie kama waliivamia Zanzibar. Ni vigumu kuvunja Muungano wa hiari.
Hivyo, wale walioapa kulinda Katiba na Muungano na sasa wanataka kuvunja Muungano huo hawalindwi na kinga za Bunge wala Uhuru wa Mawazo kwani mwanafamilia hawezi kuja na dumu la mafuta ya petroli na kiberiti mkononi na kuanza kudai kuwa pale Nyumbani watu hawampendi na hawamjali na hivyo ameamua kuichoma nyumba moto na watu wasema ati "ni uhuru wa maoni". Pale Bungeni Mbunge hawezi kusimama na kupiga kelele "moto moto" halafu watu wakikurupuka kukimbia asema "analindwa na haki na kinga za Bunge kusema lolote Bungeni".
Waondoke kwanza Bungeni na BLW ili waanzishe hoja za kuvunja Muungano; hawawezii kufanya hivyo wakiwa bado wamefungwa na viapo vya kuulinda Muungano huo.