Wanaotoka nje ya ndoa kwa fedha hawafumaniwi....!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Imebainika kwamba, ni vigumu kwa mwanaume kugundua kuwa mkewe anatoka nje ya ndoa, kama mwanamke huyo anatoka kwa ajili ya kutafuta fedha. Ni kwa sababu, wanawake wanapotoka nje ya ndoa zao kwa kuwapenda hao wanaotoka nao, hubadilika sana kihisia, kiasi kwamba, ni lazima watajiachia na kukamatwa.

Lakini wanapotoka nje ya ndoa zao kwa sababu ya fedha, hawashikwi kihisia na hivyo uwezo wa kujificha bila kufumaniwa ni mkubwa. Kinachofanya wanawake wafumaniwe ni kulewa kihisia kunakotokana na kupenda. Mwanamke anapopenda hawezi kuficha.

Lakini anapofuata fedha, anaweza kuficha hisia zake, kwa sababu hapo hakuna upendo.
Kama unatembea na mke wa mtu na huyo mwenye mke hajamshtukia mkewe, basi ujue kwamba, mwanamke huyo anakufuata kwa sababu ya fedha zako na siyo upendo.

Kwa kawaida kama mwanamke anatoka nje ya ndoa yake kwa kuwa anampenda mwanaume huyo wa nje, basi haiwezi kupita miezi sita kabla hajashtukiwa na mumewe. Huu ni ukweli unaotokana na hisia za mwanamke, kwamba, anapopenda hawezi kujizuia.
 
Naona sample ilikuwa wewe na mkeo....
 
Kweli kabisa mkuu, coz mwanamke hawezi kabisa ficha hisia, ndo mana wachache wanaweza kujiingiza kwenye mapenzi ya wanaume szaidi ya mmoja na wasigundulike
 
Kweli kabisa mkuu, coz mwanamke hawezi kabisa ficha hisia, ndo mana wachache wanaweza kujiingiza kwenye mapenzi ya wanaume szaidi ya mmoja na wasigundulike

Utakuta wenyewe wanawapanga kwa mafungu, kuna wa Vocha, kuna wa dukani, (kama sio Mangi basi atakuwa Mpemba),.....kuna wa Viwalo, (hasa hasa kama sio wauza Mitumba watakuwa wanamiliki Boutique.........), kuna wa........................ilimradi kila sekta itakuwa na mtu angalau wa kuweka mambo sawa...............LOL
 
Hili lina linawezekana baba kwa vile kupenda kunaendana na hisia ambazo zikifika zinakotakiwa kufika haifichiki kbs,but inakuwaje kwa wanaume wengi wanaokuwa na wanawake wa nje inakuwaje ni ngumu kwa wao kugundulika?
 
Wewe kweli mjasiriamali, kwa hiyo mkeo huwa anakupunguzia salio, hela ya matumizi hutoi maana mangi anasawazisha, na viwalo vya bure ndio usiseme...una raha sana, adumu mkeo kwa kuweza kuhandle familia
 
Ha ha ha haaaaaa.................kaaazi kweli kweli, ndio uzuri wa JF, ukigonga Ikulu na wewe unarudishiwa......... safi hiyo!!!!
 
Mtambuzi ya kweli haya jamani? Mkeo anaanzaje kupanga mafungu yote hayo eti huyu wa vocha, wa viwalo, wa dukani na usimgundue? ama kwenye hii post umezungumzia ambao hawajaolewa??
 
Hili lina linawezekana baba kwa vile kupenda kunaendana na hisia ambazo zikifika zinakotakiwa kufika haifichiki kbs,but inakuwaje kwa wanaume wengi wanaokuwa na wanawake wa nje inakuwaje ni ngumu kwa wao kugundulika?

Wanaume kuwagundua mbona ni rahisi sana.................... nitaweka thead ya dalili za wanaume wanaotoka nje ya ndoa zao, kama wapo humu JF wenye tabia hizo, wajue arobaini yao imefika maana kama wake zao wakisoma tu, wataanza kuwa-evaluate......................
 
kama
 
Yeah hata mimi nakubaliana na utafiti huu.............
 
mkuu huwezi kufuata pesa bila kuwa na mapenzi na kama mwanamke akitoka nje hata kama kafuata pesa lazima hisia hazitakuwepo ndani na akiipata hiyo pesa anajenga dharau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…