The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Katika halmashauri nyingi nchini imetolewa mikopo ya asilimia kumi kwa makundi ya wanawake watu wenye ulemavu na vijana. Wapo baadhi ya watu wengine wakishirikiana na baadhi ya viongozi kutoa mikopo kwa watu wasio na sifa stahiki pamoja na uwepo wa udanganyifu. Je, waliopata mikopo hii wanastahili na wamekidhi vigezo?
===
Uhakiki wa kuthibitisha vikundi vyenye sifa ya kunufaika na mikopo ya asilimia 10 katika Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, umebaini uwepo wa baadhi ya watu ambao wanafanya udanganyifu kwa kutumia miradi ya watu binafsi kuomba mikopo hiyo, jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.
Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi ya zaidi ya shilingi milioni 600 kwa vikundi 144 vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu, Afisa Maendeleo wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Wanchoke Chinchibera amesema zoezi hilo ambalo limefanywa na Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa wilaya imefanikisha kudhibiti udanganyifu huo na hivyo kutoa mikopo kwa watu wenye sifa.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Christopher Ngumbiagai amesema Serikali inatoa fedha hiyo kwa ajili ya kuwakwamua wananchi kiuchumi na hivyo kuyataka makundi yanayonufaika kutokubali kutumika katika masuala ya udandanyifu.
Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita, Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe imetoa mikopo ya zaidi ya shilingi bilioni 1.3 kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.