Wanaousaka urais, ubunge CCM kabla ya wakati waonywa

Wanaousaka urais, ubunge CCM kabla ya wakati waonywa

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
1575369935026.png

Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amewaonya wanachama wa chama hicho tawala walioanza mikakati ya kusaka kupitishwa kuwania udiwani, ubunge na urais akibainisha kuwa kufanya hivyo ni makosa.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Desemba 3, 2019 katika ziara yake kisiwani Pemba, Zanzibar wakati akizungumza na kamati ya siasa Wilaya ya Chakechake.

Dk Bashiru amesema watu wa namna hiyo hawatavumiliwa kwa kuwa taratibu za kuwania uongozi, nafasi mbalimbali katika chama hicho zipo wazi na zina muda wake.

Katibu mkuu huyo amesema wana taarifa kuwa wapo baadhi ya watu wameanza kampeni mapema wakilenga kuchaguliwa jambo ambalo halikubaliki.

Chanzo: Mwananchi
 
Mbona Magufuli kesha anza za waziwazi hajamwambia acha? Wanaccm 'hatufurahishwi' na tabia ya kujipigia debe na kumpigia wakati wapo watu kama Membe tunawazuia huku tukijua ni chaguo la wengi ndani ya chama.
Bashiru 'atuachie chama chetu' asituvuruge kabisa!
Alisikika mwana ccm asilia akiwaeleza wenzake.
 
Sheria nyingi nchi hii wametungiwa wapinzani sio Chama Tawala.!
 
Msajili wa vyama hajaliona hili na kuipa CCM onyo la kuanza mapema kampeni za Urais?
 
Back
Top Bottom