Wanaovaa nusu utupu kupigwa adhabu ya viboko

Wanaovaa nusu utupu kupigwa adhabu ya viboko

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Wananchi wa kijiji cha Ibindi, Manispaa ya Mpanda, mkoani Katavi, wamependekeza adhabu ya viboko kwa wanawake wanaovaa nguo zinazodhaniwa kuwa hazina stara, wakiunga mkono juhudi za kudumisha maadili katika jamii.

Pendekezo hili lilitolewa wakati wa mkutano wa hadhara uliofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf, ambapo aliibua masuala ya maadili na malezi kwa watoto kama njia ya kupambana na mmomonyoko wa maadili na ukatili katika jamii.

Wananchi wamesema kuwa baadhi ya mavazi ya wanawake yamekuwa kero, na hivyo wanapendekeza adhabu ya viboko kama njia ya kukomesha hali hiyo.


Chanzo: Global TV
 
Tuna waitaji VETA ili kuongeza uwezo wa kuvaa zaidi vimini
 
Back
Top Bottom