Wanapiga tena hela ya umma eti kutafuta vazi la Taifa

Wanapiga tena hela ya umma eti kutafuta vazi la Taifa

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,892
Reaction score
7,780
Hivi jamani vazi la taifa hua linatafutwa au linakuepo tu?

Mimi naamini watanzania kama taifa hatuna vazi ila tuna mavazi ya jadi kwa makabila mbalimbali ya nchi yetu. Mavazi ambayo wala hatuyavai tena isipokua kwa makabila machache kama wamasai. Wao hadi leo wameweza kudumisha uvaaji wa vazi lao la kiasili.

Kuna waziri mmoja wa utamatuni awamu ya nne alianzisha mradi wa kutafuta au kubuni vazi la taifa. Hela nyingi ikatumika mwisho wake wala vazi lilobuniwa halikukubalika na umma wa wananchi.

Nionavyo mimi mawaziri wa utamaduni waache huu mchongo wa kutafuta vazi la taifa.

Sasa waziri wa utamaduni kaanzisha tena upya eti mradi wa kutafuta au kubuni vazi la taifa. Matokeo yatakua yaleyale ya mwanzo wasanii kupewa riziki isiyokua na tija yoyote zaidi ya kua ni ubadhilifu tu.

Vazi la taifa sio kitu cha kubuniwa na wabunifu wa mavazi. Ni vazi la jadi linalotokana na utamaduni wa watu uliyojengeka kwa karne kadhaa sawa na lugha wanayoongea watu hao.

Tanzania tutambue tu mavazi ya jadi ya makabila yetu na pia ya waswahili wa pwani ya nchi yetu kama urithi wetu kimavazi. Tuachane na mradi wa kuwapa wasanii wa ubunifu ulaji huku tukijua kila watakapotuletea vazi hatutakubaliana nalo kama ndio vazi la taifa.
 
mama awe makini sana na watu wanao mzunguka naona anachukua mda sana kushtuka laaah! atashtuka wakati amesha chelewa sana
 
Masoud kipanya kawekwa kisa anajua kuchora. Mpoto kawekwa kisa anajua kutembea peku kutangaza toara.

Ngoja tuone watakuja na ubunifu gani. Ila ni jambo la kijinga sana kwa dunia ya sasa inayokuja na bunifu za mavazi kila siku.

Tena kwa jamii zetu uvaaji wetu tuu una tafsiriwa wakati mwingine na dini. So ni kitu ambacho hakina impact maana hatujawai kua nacho zaidi ya miaka 60
 
Back
Top Bottom