#COVID19 Wanasayansi: Kuchanja chanjo zaidi ya moja hakuleti madhara

#COVID19 Wanasayansi: Kuchanja chanjo zaidi ya moja hakuleti madhara

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Dar es Salaam. Wanasayansi wameondoa shaka kuwa kuchanja chanjo zaidi ya moja ni kujiletea madhara. Wamesema mtu mmoja akipata chanjo tofauti za kinga dhidi ya ugonjwa wa Uviko-19, haiwezi kumletea madhara, badala yake huongeza ufanisi wa kinga za mwili na kushambulia virusi vya corona.

Ufafanuzi huo umekuja siku chache tangu Saudi Arabia kuwataka mahujaji wanaotaka kwenda Hijja waliochoma chanjo ya Sinovac, kuchoma chanjo nyingine ambazo nchi hiyo ilizitaja kuwa ni Astrazeneca, Pfizer na Johnson & Johnson.

Akizungumza na Mwananchi juzi, Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Shadrack Mwaibambe alisema haitakiwi mtu mmoja kuchoma dozi zaidi ya moja ya chanjo ya aina moja, bali anaweza kuchanja chanjo za aina tofauti.

Alisema utafiti mwingi uliofanyika umeonyesha kuwa chanjo za aina mbalimbali zinaongeza ufanisi, kwa kuwa zimetengenezwa tofauti na zina ubora tofauti.

“Ni vizuri hakuna madhara yoyote na inafanya kazi zaidi ya moja na huleta matokeo mazuri,” alisema.

Akizungumzia hatua ya baadhi ya nchi kutaka watu wachanje chanjo wanazozitaka wao, alisema hiyo inatokana na unyanyapaa, kwamba kuna baadhi ya nchi zinaona chanjo ya aina fulani ndiyo bora.

“Ukiangalia chanjo ya Sinovac, Saudi Arabia wameikataa lakini pia ubora wake upo chini, lakini pia ni nchi husika kujikuza kwamba ipo kiwango cha juu. Hata Uingereza ina chanjo yake ambayo imekataa mataifa mengine yasizalishe. Ukiangalia kwa undani hizi chanjo zinakuja kama biashara na kila mtu anajaribu kuliteka soko.

“Uingereza walitoa kibali India izalishe, lakini sasa ukichoma ya India hawatakuruhusu uingie nchini mwao,’’ aliongeza kusema.
Dk Mwaibambe alisema suala la chanjo lina mkanganyiko mkubwa kwa Watanzania, ambao itawachukua muda kulielewa. Hata hivyo, aliwataka watu hasa wasafiri wachanje kama sharti la kwenda katika maeneo mbalimbali duniani.

Mtaalamu na mshauri wa masuala ya afya, Dk Elisha Osati alisema kuna uwezekano kwa mtu aliyechanja chanjo moja inayokinga Uviko-19, kutaka kuongeza chanjo ya pili.

Alisema kuna utafiti bado unaendelea kuhusu ufanisi zaidi, iwapo mtu atachanjwa kwa mara nyingine au ikiwa atachanganya chanjo tofauti.

“Tafiti zinaendelea lakini kuna majibu yanayoendelea kutolewa. Chanjo kama za Pfizer, AstraZeneca wanajaribu kuangalia kama inaongeza dozi kiasi gani, hatujapata majibu lakini ni jambo linalowezekana.

“Nawajua watu wamechomwa chanjo aina mbili tofauti, lakini wanaendelea vizuri tu, kikubwa tusubiri majibu yake yatatoka hivi karibuni,” alisema Dk Osati.

Kuhusu mambo yanayojitokeza ya aina tofauti za chanjo na ruhusa zake katika baadhi ya nchi, alisema hizo ni siasa, kila nchi inajaribu kupigia upatu chanjo yake.

“Ukisema Sinovac haitambuliki WHO (Shirika la Afya Duniani) inaitambua ndiyo maana imewekwa kwenye orodha ya chanjo ambazo zinaweza kutolewa. Ni siasa tu za kimatibabu zinazoingilia utaalamu,’’ alisema.

Julai 14 mwaka huu, Mwanasayansi mkuu wa WHO, Soumya Swaminathan, alishauri kuwa ni vyema kila mmoja akachoma chanjo kwa kiwango kinachofaa kulingana na dozi.

Mahujaji na chanjo
Baadhi ya Watanzania wanaotaka kwenda kuhiji, hasa waliopo visiwani Zanzibar, hivi sasa wanalazimika kuchoma chanjo kwa mara nyingine ili kuendana na masharti yaliyowekwa nchini Saudi Arabia.

Waziri wa Afya wa Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema wanaotaka kwenda Hijja ambao wamechoma chanjo hiyo awali, watalazimika kuchoma tena chanjo ya Johnson & Johnson kwa sababu Saudia haiitambui chanjo ya Sinovac.

Chanjo ya Sinovac ikiwa ni miongoni mwa zile zilizopitishwa na WHO, ilianza kutolewa Zanzibar Julai 23 mwaka huu. Hata hivyo, Saudi Arabia imesema watakaokwenda kuhiji wanatakiwa kuwa wamechomwa aina mojawapo ya chanjo kati ya tatu ambazo ni Astrazeneca, Pfizer na Johnson & Johnson.

Machi mwaka huu Saudi Arabia ilitangaza kuwa waumini wa dini ya Kiislamu watakaoruhusiwa kuhudhuria ibada ya Hijja kwa mwaka 2021 wanapaswa kuthibitisha kuwa wamepatiwa chanjo dhidi ya virusi vya corona.

Mwananchi.
 
Yote hayo ni kuogopa au kuzuia kifo?.
 
Kwa hiyo Sinovac ni sawa na nyungu yenye vyeti kwa Saudia?😁!

BTW:Wanamaanisha ni ruksa mtu mmoja kupiga collabo ya chanjo hata zote kwa mpigo (Pfizer,Astra,Sputnik,Sinovac, Abdala na J&J) na hakuna madhara? Kwa tafiti zipi au ndiyo hayo ya "nimeona watu kadhaa".

Siasa hizi! Maustadhi wakae radar,kuna Zanzibar Pilgrims Syndrome inanukia.
 
Back
Top Bottom