Wanasayansi kuunda taifa jipya anga za juu

Salahan

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2014
Posts
2,963
Reaction score
3,685
_91919926_space1.png

Kundi la wanasayansi mjini Vienna, Austria wameanzisha mpango wa kuunda taifa la amani la aina yake ambalo litakuwa na jina Asgardia.

Taifa hilo litaundwa katika eneo la anga za juu. Maelezo kwenye tovuti ya wanasayansi hao yanasema taifa hilo litakuwa nje ya udhibiti wa mataifa yoyote ya sasa na litakuwa katika mzingo wa dunia, eneo ambalo vyombo vya anga za juu huzunguka dunia.

Wanasayansi hao wanapanga kurusha satelaiti ya kwanza, ya kuanzisha taifa hilo, mwishoni mwa mwaka ujao.

Matumaini ya wataalamu hao ni kwamba siku moja hivi karibuni watatambuliwa na Umoja wa Mataifa.

Lakini baadhi ya wataalamu wanatilia shaka uwezekano wa mpango huo kufanikiwa ikizingatiwa kwamba sheria za kimataifa huzuia mataifa kudai umiliki wa maeneo anga za juu.

"Raia" wa Asgardia, ambao watachunguzwa kwa makini kabla ya kukubaliwa, mwishowe watapewa hata pasipoti, anasema Lena de Winne, mmoja wa maafisa wakuu wa mradi huo ambaye alifanya kazi kwa miaka 15 katika Shirika la Anga za Juu la Ulaya (EPA).

_91919928_space2.png

Maelfu ya watu tayari wameonyesha nia ya kutaka kujiunga na taifa hilo
Mradi huo unaongozwa na shirika la Aerospace International Research Center, ambalo lilianzishwa na mwanasayansi Mrusi, ambaye pia ni mfanyabiashara, Dkt Igor Ashurbeiyli.

Mashindano yanaandaliwa kuamua bendera na wimbo wa taifa wa nchi hiyo mpya.
Profesa Sa'id Mosteshar, mkurugenzi wa Taasisi ya Sera na Sheria za Anga za Juu ya London, amesema itakuwa vigumu kwa Asgardia kutambuliwa kama taifa ikizingatiwa kwamba haitahusiana na taifa lolote linalojitawala duniani, na pia 'raia wake' wengi watakuwa ardhini.

Tayari zaidi ya watu 50,000 wamewasilisha maombi mtandaoni kutaka kuwa raia wa taifa hilo.

Chanzo: BBC Swahili
 
Inshu ya maji wataisolve vp
hahahaha hujui hko ndo tuko karibu Na mifereji ya mvua,tuko kwny mkakati wa kuunganisha mabomba ktoka mawinguni

Halaf kuhsu umeme ndo tuko kwny mazungumzo Ili tusain mkataba Na TANESCO Ili kuwe Na umeme wa uhakika...

Tehe tehe tehe!!
 
_91919926_space1.png

Kundi la wanasayansi mjini Vienna, Austria wameanzisha mpango wa kuunda taifa la amani la aina yake ambalo litakuwa na jina Asgardia.

Taifa hilo litaundwa katika eneo la anga za juu. Maelezo kwenye tovuti ya wanasayansi hao yanasema taifa hilo litakuwa nje ya udhibiti wa mataifa yoyote ya sasa na litakuwa katika mzingo wa dunia, eneo ambalo vyombo vya anga za juu huzunguka dunia.

Wanasayansi hao wanapanga kurusha satelaiti ya kwanza, ya kuanzisha taifa hilo, mwishoni mwa mwaka ujao.

Matumaini ya wataalamu hao ni kwamba siku moja hivi karibuni watatambuliwa na Umoja wa Mataifa.

Lakini baadhi ya wataalamu wanatilia shaka uwezekano wa mpango huo kufanikiwa ikizingatiwa kwamba sheria za kimataifa huzuia mataifa kudai umiliki wa maeneo anga za juu.

"Raia" wa Asgardia, ambao watachunguzwa kwa makini kabla ya kukubaliwa, mwishowe watapewa hata pasipoti, anasema Lena de Winne, mmoja wa maafisa wakuu wa mradi huo ambaye alifanya kazi kwa miaka 15 katika Shirika la Anga za Juu la Ulaya (EPA).

_91919928_space2.png

Maelfu ya watu tayari wameonyesha nia ya kutaka kujiunga na taifa hilo
Mradi huo unaongozwa na shirika la Aerospace International Research Center, ambalo lilianzishwa na mwanasayansi Mrusi, ambaye pia ni mfanyabiashara, Dkt Igor Ashurbeiyli.

Mashindano yanaandaliwa kuamua bendera na wimbo wa taifa wa nchi hiyo mpya.
Profesa Sa'id Mosteshar, mkurugenzi wa Taasisi ya Sera na Sheria za Anga za Juu ya London, amesema itakuwa vigumu kwa Asgardia kutambuliwa kama taifa ikizingatiwa kwamba haitahusiana na taifa lolote linalojitawala duniani, na pia 'raia wake' wengi watakuwa ardhini.

Tayari zaidi ya watu 50,000 wamewasilisha maombi mtandaoni kutaka kuwa raia wa taifa hilo.

Chanzo: BBC Swahili
KAMA USHAANGALIA MOVIE INAITWA THOR ULE MJI ANAOTOKEA THOR NA KAKA YAKE UNAITWA ASGARD
 
Akili zikizidi sana mwisho huitwa ukichaa
apo ndo umemaliza kufikiria! kwa akili zako ndogo! ambaye ametengeneza sim unayotumia angekuelezea mawazo yake kabla ungemuona chiz vile vile ila saivi unaona ni jambo la kawaida, watu wako level nyingine na mpaka kutangazwa hivyo hatua zote washamaliza bado tu utekelezaji
 
Ndio mana joto linaongezeka duniani hawa wanasayansi wanachokonoa chokonoa vitu visivyochokonoleka.
 
Mwambieni bwana yule anipe nauli niende kuishi huko.TZ hapakaliki.
 
Back
Top Bottom