Ponjoro wa Kinondoni
JF-Expert Member
- Jan 5, 2024
- 3,771
- 10,311
Maelezo bila picha ni hekaya za Alfu ulela lela.Wanasayansi wanatumaini kuwa utafiti huu mpya utakuwa "mwanzo wa sayansi ya kisimi".
Hatimaye wamefanikiwa kuchora ramani ya neva za kisimi, miaka mingi baada ya ramani ya neva za uume kuchorwa, kupitia utafiti mpya ambao bado haujapitiwa rasmi na wataalamu wengine wa kisayansi (peer review).
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Amsterdam walitumia teknolojia maalumu za picha za X-ray kuunda ramani ya pande tatu (3D) ya neva za kisimi kwa wanawake wawili.
Kimsingi, mwandishi mkuu wa utafiti huo, Dr Ju Young Lee ambaye ni mtafiti katika idara ya uzazi na magonjwa ya wanawake ya Amsterdam alisema kuwa utafiti huu mpya unaweza kusaidia kuelewa vizuri jinsi kisimi kinavyofanya kazi.
Soma zaidi kupitia BBC SWAHILI
View attachment 3587193
Picha tafadhaliWanasayansi wamefanikiwa kwa mara ya kwanza kuchora ramani ya neva za kisimi, hatua inayotajwa kuwa muhimu katika kuongeza uelewa wa kisayansi kuhusu afya ya wanawake.
Utafiti huo uliofanywa na watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Amsterdam nchini Uholanzi ulitumia teknolojia maalumu ya picha za X-ray kuunda ramani ya pande tatu (3D) ya neva za kisimi kwa wanawake wawili.
Kwa mujibu wa mwandishi mkuu wa utafiti huo, Dkt. Ju Young Lee, ambaye ni mtafiti katika idara ya uzazi na magonjwa ya wanawake ya chuo hicho, mafanikio hayo yanaweza kusaidia wataalamu kuelewa kwa undani zaidi jinsi kisimi kinavyofanya kazi na kuchangia maendeleo ya tafiti za afya ya wanawake.
Watafiti wana matumaini kuwa matokeo hayo yatakuwa mwanzo wa enzi mpya ya tafiti zinazolenga kuelewa vyema muundo na kazi za kisimi, eneo ambalo kwa muda mrefu limekuwa halijafanyiwa utafiti wa kina ikilinganishwa na viungo vingine vya uzazi.
Ingawa utafiti huo bado haujapitiwa rasmi na wataalamu wengine wa kisayansi (peer review), umeibua mjadala mpana katika jamii ya wanasayansi kuhusu umuhimu wa kuongeza utafiti katika afya ya wanawake.
Chanzo: BBC News Swahili
Umoja wa wanaume tumetoa ruhusaPicha ya kisimi iko wapi kwa wasiokijua?
Ama kama vipi mkiniruhusu napiga picha hapa naweka
🤣🤣🤣🤣Umoja wa wanaume tumetoa ruhusa
dronedrake , Mbaga Jr andaeni mafuta.Picha ya kisimi iko wapi kwa wasiokijua?
Ama kama vipi mkiniruhusu napiga picha hapa naweka
Itafaa kuisomea, fani mpya itakayoibuka ya clitoris specialists.Sawa mwishoni atapatikana Dr wake wa hiyo sehemu tuuu
Poor Braindronedrake , Mbaga Jr andaeni mafuta.
Aiseee !!! 😀Picha ya kisimi iko wapi kwa wasiokijua?
Ama kama vipi mkiniruhusu napiga picha hapa naweka
Mboga Za Majanineva ya kisimi ila picha ya majani, ndo nini sasa