Wanasayansi wagundua njia ya kuangamiza malaria duniani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363

Mbu aenezae Malaria.

KWA UFUPI
Moja ya tahadhari ambayo wanasayansi hao wanaichukua, taarifa hiyo inasema ni kuzuia kimelea wa malaria kujijengea usugu dhidi ya bakteria, Wolbachia..

Dar es Salaam. Wanasayansi nchini Marekani wamegundua aina ya bakteria ambao wana uwezo wa kumfanya mbu awe na kinga dhidi ya vimelea vya malaria.

Kwa kawaida mfumo wa maisha wa vimelea wa malaria hukamilika kwa kuishi kwa mbu na binadamu.

Ugunduzi huo wa wanasayansi utakatisha maisha ya vimelea hao wa malaria wanaofahamika kama Plasmodium na kuweza kuufanya ugonjwa huo unaoongoza kwa kuua watu wengi duniani uwe ni historia.

Wanasayansi hao kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyosambazwa kupitia mtandao na Taasisi ya Kukabiliana na Magonjwa ya Mzio na Kuambukiza (NIAID),wameeleza kuwa ugunduzi huo unaweza kuzima kabisa tabia ya mbu ya kumwambukiza binadamu ugonjwa wa malaria.

Katika ugunduzi huo ulioongozwa na Dk Zhiyong Xi wa Chuo Kikuu cha Michigan walifanikiwa kubaini dawa itakayotumika kama chanjo kwa mbu anayeeneza malaria ili imfanye atengeneze kinga ya kutokuruhusu vimelea vya malaria kuishi kwenye mwili wake.

Wakijua fika kwamba kimelea wa malaria huanza kuishi kwa mbu aina ya Anopheles kabla ya kuambukizwa kwa binadamu anapomuuma, waliona hiyo ni njia pekee ya kuumaliza ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, walimtaja bakteria anayefahamika kama Wolbachia kuwa ana uwezo wa kuzuia maendeleo ya Plasmodium kwenye mwili wa mbu.

Kulingana na ugunduzi huo wana uwezo wa kutumia utaalamu wao katika kumfanya bakteria Wolbachia aishi kwa mbu anopheles. Mbu anayeishi na bakteria huyo wa Wolbachia ataweza kukifanya kizazi chake chote kiishi na bakteria huyo.

Ugonjwa wa malaria unaongoza kwa kuua idadi kubwa ya wat duniani.


Wanasayansi wagundua njia ya kuangamiza malaria duniani - Kitaifa - mwananchi.co.tz









 
maskini plasimodium.
Niliwahi kufundishwa economic importance of malaria,SASA DOKTA WATAKULA WAPI,si watakufa njaa,tena magonjwa mengi yakipata tiba,sipati picha
 
maskini plasimodium.
Niliwahi kufundishwa economic importance of malaria,SASA DOKTA WATAKULA WAPI,si watakufa njaa,tena magonjwa mengi yakipata tiba,sipati picha
Mkuu Mshinga Ma-Daktari watakuwa wanakwenda kazini kulala usingizi kwenye ofisi zao kwa sababu Dawa kila siku zinapatikana kutibu Magonjwa sugu duniani wana sayansi wanazidi kuvumbuwa madawa kila kukicha kazi kwao hao Ma Daktari wamekalia kuti kavu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mshinga Ma-Daktari watakuwa wanakwenda kazini kulala usingizi kwenye ofisi zao kwa sababu Dawa kila siku zinapatikana kutibu Magonjwa sugu duniani wana sayansi wanazidi kuvumbuwa madawa kila kukicha kazi kwao hao Ma Daktari wamekalia kuti kavu.
Ugunduzi huo ni kwa ajili ya kutengeneza faida nono(kunenepesha mifuko ya mabepari) tu.


Usisahau na hii
NWO Plans To Depopulate The Earth

Connecting the Dots: Mass depopulation on its way and the Secret Team's management of the world -- Society's Child -- Sott.net
 
Last edited by a moderator:
 
Last edited by a moderator:
Aisee.
Sio doctors pekee, hata watafiti wataathirika.

A great approach i should say. Kwa sababu kuondoa mazalia ya mbu imekuwa issue basi kumbe kuattack host inawezekana.
maskini plasimodium.
Niliwahi kufundishwa economic importance of malaria,SASA DOKTA WATAKULA WAPI,si watakufa njaa,tena magonjwa mengi yakipata tiba,sipati picha
 
hahaha kweli sector zinategemeana kila mmoja anapendelea au anavutia kwake kazi kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…