Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Wanasayansi nchini Uzbekistan wanatengeneza chanjo dhidi ya virusi vya corona inayoweza kuliwa ndani ya nyanya, Wizara ya Ubunifu ya nchi hiyo imeeleza.
Wanasayansi kutoka Chuo cha Sayansi wamefanikiwa kuweka sehemu ya kirusi hicho ndani ya seli ya nyanya ambapo seli hiyo imegeuka kuwa chanjo dhidi ya virusi hivyo.
Jaribio hilo linatarajiwa kukamilika baada ya kukuza nyanya kwa miezi miwili ambapo watu watakaokula nyanya hizo watatengeneza kinga ya mwili dhidi ya virusi vya corona.
Msemaji wa Chuo hicho ameliambia Shirika la Habari la Uturuki (Anadolu Agency) kuwa majaribio ya chanjo hiyo yalianza mwezi Januari na kuwa chanjo hiyo kwa sasa inajaribiwa kwa wanyama.
Hatua ya kwanza ya majaribio ya chanjo kwa binadamu itaanza mara tu majaribio kwa wanyama yatakapokamilika.
Chanzo: AA