Wanasayansi watengeneza kinga mpya ya mwili inayoweza kushambulia 99% ya HIV

amanda cute

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2016
Posts
244
Reaction score
456
Wanasayansi wamekuwa wakitengeneza chembe chembe za kinga ya mwili zinazoweza kushambulia asilimia 99% ya virusi vya HIV vinavyosababisha ukimwi na hivyo kuzuwia maambukizi kuendelea.

Chembe chembe hiyo ya kinga imetengenezwa kwa ajili ya kushambulia sehemu tatu muhimu za virusi na hivyo kuvifanya virusi hivyo kushindwa kuhimili mashambulizi yake.

Kazi ya utengenezaji chembe chembe hizo za kinga ya mwili imetokana na ushirikiani baina ya Taasisi ya Marekani ya Afya na kampuni maduka ya dawa ya Sanofi.

Shirika la kimataifa la kukabiliana na ukimwi -International Aids Society linasema kuwa huu ni "ugunduzi wa kihistoria ".

Yeyote mwenye HIV kupata tiba Afrika Kusini

Mwanamume mwenye HIV aliyefanya mapenzi na wanawake 104 Malawi

Dawa za kupunguza makali ya HIV

Majaribio ya kinga kinga hiyo ya mwili kwa binadamu yataanza kufanyika mwaka 2018 kuangalia kama dawa hiyo inaweza kuzuwia ama kutibu maambukiziya HIV

Miili yetu huhangaika kupigana na virusi vya HIV kwasababu virusi hivyo vina uwezo mkubwa wa kujibadilisha katika hali nyingine pamoja na muonekano wake.

Aina kadhaa za virusi vya HIV - katika mgonjwa mmoja zinaweza kufananishwa na zile za mafua wakati wa msimu wa baridi.

Kwa hiyo mfumo wa kinga ya mwili najipata katika vita dhidi ya magonjwa kadhaa nyemelezi yanayosababishwa na HIV.

Lakini baada ya miaka kadhaa ya maambukizi, wagonjwa wachache hujenga silaha kali ya mwili ambapo " Mwili hupunguza uharibifu wa kinga ya mwili " kwa kushambulia kwa kiasi kikubwa maambukizi ya HIV.

Watafiti wamekuwa wakijaribu kutumia uwezo wa mwili wenyewe wa kupunguza uharibifu wa kinga ya mwili kama njia ya kutibu HIV, ama kuzuwia maambukizi hayo mapema.

CHANZO: BBC
 
please please wana JF ni vema also tukawa ni jukwaa zuri kuelezea kuhusu hili suala,AIDS IPO na madhara yake bado ni makubwa mno,sio suala la kulifanyia masihara,kinga bado ni muhimu mno na jamii iendelee kuelezwa hivyo,waziri wangu wa Afya yupo kimya kabisa kuhusu suala hili,inaelekea naye analichukulia kisiasa,wenzetu wapo very serious na wanajitahidi mno kuelimisha wananchi wao pamoja na kuwapa dawa za kusaidia kurefusha maisha,wanafanya tafiti nyingi mno ,sisi bado tumelala,AIDS ITS NOT A JOKE
 
Kenya wapo vizuri sana
 
Jamani wanajf tusifanye masihala kwenye hili hiyo issue Sikia kwa mwingine tuu lisikukute
 
HIV ni kitu kingine wakuu, kuna chuo kule iringa waligundua dawa ya ukimwi kwa mtu ambae hajaanza kutumia madawa! Dose yake ni lita kumi, imagine unakunywa dawa lita kumi[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Wangeitangaza nasisi gungeingia kwenye Guinness book of records
 
HIV ni kitu kingine wakuu, kuna chuo kule iringa waligundua dawa ya ukimwi kwa mtu ambae hajaanza kutumia madawa! Dose yake ni lita kumi, imagine unakunywa dawa lita kumi[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Wakatibu wangap? Achakutudanganya
 
Mim hiyo kinga kupewa ntaisubiria airpot kabisa,,kondom mbayaa
 
HIV ni kitu kingine wakuu, kuna chuo kule iringa waligundua dawa ya ukimwi kwa mtu ambae hajaanza kutumia madawa! Dose yake ni lita kumi, imagine unakunywa dawa lita kumi[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Lita kumi kwa siku ay?[emoji23][emoji23][emoji23] umenifanya nicheke kama mazuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…