Wanasheria ambao hawajaenda Law School wasiendeshe mashitaka

Wanasheria ambao hawajaenda Law School wasiendeshe mashitaka

cheguevara

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2012
Posts
1,348
Reaction score
652
Kumekuwa na tabia ya baadhi ya taasisi zinawatumia wanasheria ambao hawajaenda law school wakati wameajiliwa muda mrefu na wamekuwa wakiomba kwenda kujiendeleza lakini hawapewi nafasi hiyo hata kama wameomba kwenda kujisomesha wao wenyewe.

Ni jambo la msingi sasa idara ya mahakama iwazuie hadi wamalize/wapelekwe law school kwani hii ni kuwanyima haki yao ya msingi na kuwabana wasiweze kubadili mwajiri kwenda kutafuta maslahi bora na utendaji ulio bora.

Ikiwezekana Chama Cha Wanasheria Tanzania kiingilie katika hili kwani ni kudumaza tasinia ya sheria.
 
sio kwenda law school ni kufaulu hiyo law school.

huwezi kufaulu lawschool bila kuudhulia lawschool,kwanza uudhulie au upelekwe/uruhusiwei na mwajiri wako kufaulu/kufeli ni matokeo tu
 
kabla ya law school hakukua na shughuli za kisheria??. Mengine ni urasimu na usumbifu tu.
 
heading na Content kwenye thread iliyoko mbele yetu haijakaa sawa.
Sasa kama wanaomba waende Law School na wananyimwa kwanini wazuiliwe kuendesha mashitaka! na ukizingatia kwamba wameishafanya kazi kwenye Field hiyo ya Sheria kwa Muda, ni kipi wanakuwa hawakijui???? Law School ni kwenda kupata mbinu in Legal Practice of which hao wa makazini wanakuwa nazo tayari.
 
Kumekuwa na tabia ya baadhi ya taasisi zinawatumia wanasheria ambao hawajaenda law school wakati wameajiliwa muda mrefu na wamekuwa wakiomba kwenda kujiendeleza lakini hawapewi nafasi hiyo hata kama wameomba kwenda kujisomesha wao wenyewe.

Ni jambo la msingi sasa idara ya mahakama iwazuie hadi wamalize/wapelekwe law school kwani hii ni kuwanyima haki yao ya msingi na kuwabana wasiweze kubadili mwajiri kwenda kutafuta maslahi bora na utendaji ulio bora.

Ikiwezekana Chama Cha Wanasheria Tanzania kiingilie katika hili kwani ni kudumaza tasinia ya sheria.
mahakama haiwezi kuwazuia wanasheria kuendesha mashitaka. mawakili wa serikali wote wamepitia training nyingi sana na wana uzoefu wa kutosha. ajabu yake ni kwamba, hata ukimaliza lawschool na kufaulu, ukiingia ofisi ya mwanasheria mkuu ukawa prosecutor bado unahitaji training nyingi sana, ile ya lawschool tu ni more of theory na utafanya kazi karibia mwaka mmoja na zaidi ndio utakuwa convesant na taratibu za kuendesha mashitaka.

vilevile, ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali siku hizi hawaajiri wanasheria wasiopitia lawschool. hivyo usiwe na shaka. inavyoonekana wewe ni mwanafunzi bado hujamaliza shule ya sheria, usipomaliza shule ukafaulu na kupata cheti hauwezi kuajiriwa kama wakili wa serikali, plus intenship juu. unaweza kupata kazi kama hakimu mkazi lakini wakili wa serikali hupati. mwenye mamlaka ya kuajiri walio na cheti cha lawschool au la ni mwanasheria mkuu sio mahakama.

vilevile, vijana wa siku hizi msijione mmemaliza lawschool mkafikiri mko vizuri kuliko wale malawyer wa zamani. kama ni hivyo basi tusema wanasheria wengine wooote hapa dsm ambao hawajaenda lawschool hata hao mnaopitapita na bahasha kuomba kujishikiza kabla hamjapata kazi, tuseme sio wazuri kwasababu hawakupitia lawschool?hahaha. noo. ukija kwenye field na kiburi cha lawschool kama hicho utapata shida sana na utakata tamaa maana utakutana na mauzoefu ya practice huku na utajikuta mweupe kabisa.
 
nenda mtaani kakutane nao hao ambao hawajaenda lawschool lakini wamekuwa kwenye practice kwa miaka mingi na wamefaulu mtihani wa bar na kuthibitishwa kuwa mawakili wa kujitegemea....utashangaaa. lawschool ni nzuri lakini bado unahitaji training nyingine nyingi sana ili uwe mwanasheria. hapo bado sana dogo. hao walimu wako wanaokufundisha hapo chuo tu tunawapiga chini sana kesi, tunawashinda huku mtaani. we waulize watakwambia.
 
Kwanza,tambua ya kuwa Law School of Tanzania si kwa kila Mwanasheria wa nchi hii.Hii ni kwakuwa Sheria iliyoanzisha Taasisi hiyo inawataka wahitimu wa sheria wa mwaka 2008 na kuendelea kwenda katika Taasisi.Hivyobasi, kuanzia 2007 kushuka chini,hawapaswi kwenda LST.Pili, masomo serikalini yana taratibu na sifa zake. Tatu, si kila anayeomba masomo anaruhusiwa kusoma.
 
Back
Top Bottom