Borro
Member
- Nov 29, 2011
- 98
- 40
Mzee wangu alikua na kesi na mama mmoja hivi mahakama ya mwanzo. Huyu mama alikuja nyumbani kwetu kuomba msaada tumuhifadhie gari yake hiace kwa sababu kuna uzio, kwa muda wa wiki mbili maana ni jirani yetu, na hii ilikua ni muda mfupi tu baada ya kufiwa na mme wake akidai hakua na msimamizi makini na mara baada ya kumpata msimamizi ndani ya wiki mbili angekuja kutoa gari yake. Sasa kilichotokea ni kwamba huyu mama hatukumuona ndani ya hizo wiki mbili, alikuja kuonekana baada ya miaka miwili na tulipomueleza suala la kutoa gari kwetu aligoma katakata akidai kwamba kuna baadhi ya vitu havipo mpaka tumlipe pesa kufidia hivyo vitu ndo atoe gari, anyway madai yake yalikua ya kutunga tu ili apige pesa.
Ilibidi mzee afungue kesi mahakama ya mwanzo akiiomba mahakama itoe amri huyu mama atoe gari yake nyumbani kwetu. kwa kuona vile huyo mwanamke nae akafungua kesi mahakama hiyo hiyo akidai alipwe pesa kufidia vifaa vya gari anavyosema havipo. kesi ilianza kusikilizwa toka Jan 2013 hadi August, hukumu ikatoka kwamba huyu mwanamke atoe gari yake kutoka kwetu ndani ya mwezi mmoja kuanzia siku ya hukumu. Mwezi umeisha jana na hakuna taarifa yoyote kuja kwetu kutoka mahakama kesi ilipoamuliwa kama huyo mwanamke alikata rufaa, lakini pia gari bado ipo nyumbani hajaitoa.
Leo nimecheki na mzee wangu kaniambia kuna barua ameletewa na mjumbe wa nyumba kumi, akihitajika mahakama ya wilaya kwa ajili ya kusikiliza shauri kuhususiana na madai ya huyo mama. Lakini pia leo hii mzee alienda mahakamani ( ya mwanzo) kupata kibali rasmi cha kuiondoa hiyo gari hata kwa gharama zetu baada ya muda wa mwezi mmoja aliokua amepewa huyo mwanamke kuondoa gari yake kuisha. Hakimu kamueleza mzee kwamba huyo mwanamke hakuwahi kwenda mahakamani kwa ajili ya taratibu za kukata rufaa, lakini yeye kaondoka moja kwa moja kwenda mahakama ya wilaya na kuchukua barua ya mzee kuitwa mahakamani.
Sasa wanasheria,
1. Naomba kujua taratibu za kukata rufaa kwenda mahakama ya juu zikoje?, na huyu anayekata rufaa ni taratibu zipi anazotakiwa kuzikamilisha kutoka mahakama iliyotoa hukumu ndo rufaa aipeleke mahakama ya juu?.
2. kwa mfano huyu mwanamke kama atakua amekiuka utaratibu na ikizingatiwa kwamba muda aliopewa ndani ya mwezi mmoja awe amekata rufaa hakukata na huo muda tayari ushaisha, lakini pia yeye kakimbilia mahakama ya wilaya kuchukua barua ya kuanzisha mashitaka upya, kisheria hiyo kesi ipo na uhalari wa kusikilizwa au haina?.
3. Huyu mwanamke amekataa kutoa gari yake kutoka kwetu pamoja na kuwa ameamuliwa na mahakama, je siye tunaweza kuivuta na kuipeleka kwake?, awepo au asiwepo kwake? au kwenye suala zima la kuondoa gari tuipeleke wapi?. Ndugu zangu wanasheria naombeni sana msaada wa ufafanuzi kwa hayo maswali yangu.
Thanks JF, the platform of great thinkers.