Wanasheria JF Naomba kujua au Ufafanuzi kwa Hili.

Borro

Member
Joined
Nov 29, 2011
Posts
98
Reaction score
40
Mzee wangu alikua na kesi na mama mmoja hivi mahakama ya mwanzo. Huyu mama alikuja nyumbani kwetu kuomba msaada tumuhifadhie gari yake hiace kwa sababu kuna uzio, kwa muda wa wiki mbili maana ni jirani yetu, na hii ilikua ni muda mfupi tu baada ya kufiwa na mme wake akidai hakua na msimamizi makini na mara baada ya kumpata msimamizi ndani ya wiki mbili angekuja kutoa gari yake. Sasa kilichotokea ni kwamba huyu mama hatukumuona ndani ya hizo wiki mbili, alikuja kuonekana baada ya miaka miwili na tulipomueleza suala la kutoa gari kwetu aligoma katakata akidai kwamba kuna baadhi ya vitu havipo mpaka tumlipe pesa kufidia hivyo vitu ndo atoe gari, anyway madai yake yalikua ya kutunga tu ili apige pesa.
Ilibidi mzee afungue kesi mahakama ya mwanzo akiiomba mahakama itoe amri huyu mama atoe gari yake nyumbani kwetu. kwa kuona vile huyo mwanamke nae akafungua kesi mahakama hiyo hiyo akidai alipwe pesa kufidia vifaa vya gari anavyosema havipo. kesi ilianza kusikilizwa toka Jan 2013 hadi August, hukumu ikatoka kwamba huyu mwanamke atoe gari yake kutoka kwetu ndani ya mwezi mmoja kuanzia siku ya hukumu. Mwezi umeisha jana na hakuna taarifa yoyote kuja kwetu kutoka mahakama kesi ilipoamuliwa kama huyo mwanamke alikata rufaa, lakini pia gari bado ipo nyumbani hajaitoa.
Leo nimecheki na mzee wangu kaniambia kuna barua ameletewa na mjumbe wa nyumba kumi, akihitajika mahakama ya wilaya kwa ajili ya kusikiliza shauri kuhususiana na madai ya huyo mama. Lakini pia leo hii mzee alienda mahakamani ( ya mwanzo) kupata kibali rasmi cha kuiondoa hiyo gari hata kwa gharama zetu baada ya muda wa mwezi mmoja aliokua amepewa huyo mwanamke kuondoa gari yake kuisha. Hakimu kamueleza mzee kwamba huyo mwanamke hakuwahi kwenda mahakamani kwa ajili ya taratibu za kukata rufaa, lakini yeye kaondoka moja kwa moja kwenda mahakama ya wilaya na kuchukua barua ya mzee kuitwa mahakamani.
Sasa wanasheria,
1. Naomba kujua taratibu za kukata rufaa kwenda mahakama ya juu zikoje?, na huyu anayekata rufaa ni taratibu zipi anazotakiwa kuzikamilisha kutoka mahakama iliyotoa hukumu ndo rufaa aipeleke mahakama ya juu?.
2. kwa mfano huyu mwanamke kama atakua amekiuka utaratibu na ikizingatiwa kwamba muda aliopewa ndani ya mwezi mmoja awe amekata rufaa hakukata na huo muda tayari ushaisha, lakini pia yeye kakimbilia mahakama ya wilaya kuchukua barua ya kuanzisha mashitaka upya, kisheria hiyo kesi ipo na uhalari wa kusikilizwa au haina?.
3. Huyu mwanamke amekataa kutoa gari yake kutoka kwetu pamoja na kuwa ameamuliwa na mahakama, je siye tunaweza kuivuta na kuipeleka kwake?, awepo au asiwepo kwake? au kwenye suala zima la kuondoa gari tuipeleke wapi?. Ndugu zangu wanasheria naombeni sana msaada wa ufafanuzi kwa hayo maswali yangu.

Thanks JF, the platform of great thinkers.
 
Wakati mnakabidhiana gari kulikuwa na ushahidi wa kimaandishi? Kama ulikuwepo ulikuwa unasemaje? Kama haukuwepo una uhuru wa kujimilikisha hiyo gari au kuifanya vyovyote ukiona bado huyo mama anawafuata fuata unaweza ukampiga na kiyu chenye ncha kali...hahhaahaha
 
Mzee mng'oa kucha, kipindi analeta hiyo gari hatukuandikiana chochote katika makabidhiano, yaani ni ile huruma tu kwa huyo mwanamke kufuatia kufiwa na mme wake ndo ilipelekea kumuamini na kutokua na shaka kama angeweza kubadilika. Kwa ufupi mkuu huyo mwanamke ni msanii na tapeli pia, anataka kupiga pesa mchana kweupe lakini kesi tushamshinda maana tayari. Kuhusu kujimilikisha hiyo gari yake siye hatuna huo mpango kabisa tunachohitaji tu ni yeye kuondoa gari yake home. Kumpiga na kitu chenye ncha kali hatakuja kutokea ni bora tukamlipa pesa anayodai kuliko kufanya dhambi kama hiyo, ingawa huyo mama kishatucost sana na hiyo kesi ambayo mie naina ni usumbufu usiokua na maana. However thanks kwa comment mzee, ingawa hukunifafanunulia zaidi kuhusu maswali niliyouliza.
 
huyo ama ana haki ya kukata rufaa endapo anahisi maamuzi ya mahakama ya mwanzo yana upungufu/uonevu, kinachopaswa ni ushahidi wenu na wake kuonyesha kuwa mnayojitetea ni kweli, onluy ushahidi, baada ya kesi nanyi mnaweza kumfungulia kesi kwa usumbufu aliowapa na gharama zisizo na lazima.
 
Ngoja walio soma CIVIL PROCEDURE LAW waje wakupe majibu
ila kwa kugusia tu(me sio mtaalam kwenye madai)
swali namba
1. ambaye hajalizika na maamuzi lazma Auchukue LEAVE OF THE COURT kutoka mahakama iliyotoa hukumu
2. kama hakukata rufaa inamaana hapo hamna kesi coz '' you cant file a new case whch has been already decied by another Court of law concerning the same PARTIES, facts, nature and material unless its an appeal originating from a surbodinate court'' Unachotakiwa ni cku ile ya kesi hyo mpya we nenda na vithibitisho(copy ya judgement+injuction order ya mahakama) kuonesha kwamba kesi hiyo imeshafanyiwa maamuzi (RES JUDICATA) as per section 9 of the CIVIL PROCEDURE CODE [CAP 33 R.E 2002]..kama kweli hakimu aliwaambia hakukata rufaa(maana lazma apate leave of the court) baasi fanyeni kma nlivyojaribu kuainisha hapo.

3. kama hakukata rufaa basi hapo atakuwa amekaidi AMRI halali ya Mahakama jambo ambalo ni kosa ... USHAURI baada ya hayo yote kuisha na kufahamika atoe au vp ,,,kutokana na usumbufu aliowapatia na ujanja alioufanya nyie nanyi Mfungulieni kesi ya madai
(1)fidia ya garama za kumtunzia gari lake (kutokea siku BAADA YA WIKI 2 ZA MAKUBALIANO)maana kma angeweka garage angelipia
(2)fidia ya usumbufu aliowasababishia (kutokea kutunza gari mpaka garama ya kesi zake zisizo na msingi
(3)kama kuna madhara yoyote yaliyotokana na gari lake mf. financial loss(kma uliwahi kulifanyia repair)
sjui kma ntakua nmekujbu vya kutosha
 
Nina swali kabla sijakupa ushauri wangu:
1. Ile kesi aliyofungua yeye Kudai kulipwa vifaa vyake vilivyopotea iliishaje?
Kwa kawaida notice ya appeal huombwa kwenye mahakama iliyotoa uamuzi. Kwa mantiki ya kesi yako ilibidi notice iombwe Primary kwenda District court. Sasa kama hakimu kashamweleza mzee wako kua yule Mama hakufile appeal notice bas hamwez kujua huko District mnaitiwa nini. Mwache kwanza mzee wako aende akasikie ni shaur gan anaitiwa then kama litakua ni shaur lile lile la primary court mtakua na substantive objection za kutosha kwenye point of law
1. Res judicata kama alivyosema mdau hapo juu
2. Failure to file appeal notice which means the matter is already bared from further hearing. ( hii ni incurable )
Otherwise una lolote feel free to ask.
 
Mzee "Nyakubi'' samahani nahisi kama waweza kuwa poti hivi, hahahahahaha hahahahahaha. kwa kweli nashukuru sana kwa kunipa majibu mazuri sana yenye weredi hasa wa kisheria. Nilikua na wasiwasi na fikira zangu kwa jinsi ninavyojua kuhusu rufaa, lakini kwa kweli umeniongezea nondo za kutosha sana na siku mzee atakapoenda mahakama ya wilaya kama mahakimu watatenda haki basi kesi na huyo mwanamke inaweza kuisha. Kwa sasa mie sipo nyumbani nipo mbali na sitaweza kuhudhuria lakini mzee nitamcheki na kumuongezea huu ushauri ulionipa.
Mzee tayari kishamfunguliaa kesi ya madai na usumbufu mwingine na ishapangiwa tar ya kusikilizwa. Pia mzee yupo kwenye mchakato wa kupata hiyo copy ya hukumu, si unajua tena mahakama zetu urasimu kibao lakini tutajitahidi kupata hivyo vielelezo vyote kabla ya tarehe ya kusikiliza kama ni rufaa au kitu gani.
Thanks mkuu for your contribution over my request and God bless you.
 
thanks pia! POTI ndo nn mkuu
 
Mkuu Mosaad007,

kwanza nakushukuru sana kwa ufafanuzi wako mzuri, for sure I real mean it broda. Ile kesi aliyofungua huyo mwanamke kudai tumlipe baadhi ya vifaa kwenye gari, mahakama ilijidhihirisha pasipo shaka kwamba alikua anataka kututapeli ili apige pesa hivyo ''alishindwa''. Na mahakama iliamua aondoe gari yake kutoka kwetu ndani ya mwezi mmoja laakini hakufanya hivyo na maatokeo yake ndo kaibukia mahakama ya wilaya.
Labda nikupe maelezo kidogo, Mzee alifungua kesi ya kuiomba mahakama itoe amri gari ya huyo mwanamke aiondoe, ambapo pasipo na shaka iliona yule mwanamke ni tapeli na ikaamuaa gari aiondoe. Lakini pia naye huyo mwanamke alifungua kesi akiiomba mahakama itoe amri tumlipe pesa kwa vifaa anavyosema vilipotea, mahakama iliona kwamba yule mwanamke alikua anadanganya hivyo ikasema hawezi kulipwa. So baada ya hayo yote gari hajatoa na ndo kakimbilia mahakama ya wilaya, ndo sijajua kama ni rufaa au kajichanganya kafungua kesi mpya.
Kingine mkuu nilitaka kujua, kwa kuwa mahakama ilikua imeamua gari iwe imeondolewa kutoka kwetu ndani ya mwezi mmoja na baada ya huo muda gari bado ipo:
1. Je siye kwa upande wetu tunaweza kuitoa kwa gharama zetu?.

2. Na nini kinatakiwaa kifanyike kwanza kisheria au kutoka mahakama iliyotoa hukumu ndo tuwe na mandate ya kuitoa hiyo gari kutoka kwetu?.

3. Hivi ni wakati gani copy ya hukumu inatakiwa iwe imetolewa kwa mhusika kwa ajili ya reference hasa katika suala zima la rufaa?.

4. Hakimu aliye amua hiyo kesi alishauri gari tusiiondoe kwanza kutoka home hadi mzee wangu atakapokua ameenda kusikiliza nini ameitiwa mahakama ya wilaya, je hakimu alikua sahihi au naye alipotoka kiaina?, maana mie nilidhani hata kama huyo mwanamke angekata rufaa hukumu ya mahakama kuondoa gari ingebaki kama ilivyo kwa utekelezaji na hata kama maamuzi ya rufaa yakitokaa baadae bado gari ilitakiwa iwe emetoka kwetu maana siyo yetu.

Kaka nakushukuru sana na pia nakuomba usichoke kunisaidia ufafanuzi zaidi kwa hayo maswali yangu hapo juu.

Thanks broda and God bless you.
 
Nameless Girl, thanks kwa ushauri wako bidada.
Kuhusu ushaidi kwa kweli mahakama ilikua na uvumilivu wa hali ya juu sijapata kuona labda pengine haka kamwanamke kalikua kanajinasibu kajane, maana alipewa muda mara nyingi sana kuleta mashahidi ambao yeye mwenye alisema anao lakini cha ajabu kila wakati alipotakiwa alete mashaidi hakuna hata mara moja shaidi alikuja mahakamani. Kiukweli, huyu mwanamke lengo ilikua ni kupiga pesa tu kwa kutumia mgongo wa ujane na pia uwaminifu wetu, kulikua hakuna upotevu wowote wa vifaa kutoka kwenye gari yetu, ni ushetani tu kwa baadhi binadamu kwa dunia ya leo.
Mzee tayari kishafungua kesi ya madai kwa kumtunzia gari yake kwa muda huo wote.

Thanks bidada.
 
"POTI ndo nn mkuu"?.
Mzee Nyakubi usiogope kaka, hahahahahahaha hahahahahahahaha. Mara nyingi wenyeji wa mkoa wa mara wanapokutana nje ya mkoa wao hutambulishana kwa kuitana POTI. So hiyo usaname yako (NYAKUBI) imekaa kimkoa wa mara mara hivi, "and for sure its a typical jita name'', nami origin yangu ni huko mara, so usijali kaka.
Anyway mkuu pia kwa ufupi kama una muda unaweza kurespond kwa ufafanuzi katika maswali yangu hapa chini?.

1. Je siye kwa upande wetu tunaweza kuitoa kwa gharama zetu?.

2. Na nini kinatakiwaa kifanyike kwanza kisheria au kutoka mahakama iliyotoa hukumu ndo tuwe na mandate ya kuitoa hiyo gari kutoka kwetu?.

3. Hivi ni wakati gani copy ya hukumu inatakiwa iwe imetolewa kwa mhusika kwa ajili ya reference hasa katika suala zima la rufaa?, maana naona kama hakimu aliyeaamua kesi yetu hana haraka sana na hata anapoombwa inaonekana hajali vile.

4. Hakimu aliye amua hiyo kesi alishauri gari tusiiondoe kwanza kutoka home hadi mzee wangu atakapokua ameenda kusikiliza nini ameitiwa mahakama ya wilaya, je hakimu alikua sahihi au naye alipotoka kiaina?, maana mie nilidhani hata kama huyo mwanamke angekata rufaa hukumu ya mahakama kuondoa gari ingebaki kama ilivyo kwa utekelezaji na hata kama maamuzi ya rufaa yakitokaa baadae bado gari ilitakiwa iwe emetoka kwetu maana siyo yetu.

5. Mahakama iliamua gari itolewe kwetu ndani ya mwezi na kipindi hicho tayari kishapita, je sisi tunaweza kuivuta na kuipeleka kwake?, na je kisheria tutakua sawa?, au maamuzi yeyote ya kuiondoa gari kutoka kwetu ni lazima tusubiri uamuzi wa mahakama tena kuhusu rufaa?.

Samahani sana mzee kwa muda wako lakini kama utakua kwenye position ya kunifafanulia hayo maswali yangu hapo juu nitashukuru sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…