Kwa nini asiwalipe kupitia simu zao za mikononi hata kama wako porini?
Wakuu bosi wangu anataka kuniweka matatani kwa kunibebesha fedha kiasi kikubwa kupelekea wafanyakazi mishahara site sasa tumekaa na nimeona ananiweka kwenye risk kubwa ya kuvamiwa na kuibiwa au kupoteza uhai
wanasheria nisaidieni kifungu cha sheria kinachombana mwajiri kulipa mfanyakazi mshahara kupitia benki ili nikiweke hapa kwenye barua ya kumlazimisha kutoka kwa wafanyakazi walio hapa site
Wanasheria na Ma HR msaada wenu
Sent using Jamii Forums mobile app
Jenga hoja, syo lazima iwe ktk sheria.. Pia hakuna sheria inayolazimisha kulipa mshahara kwa benk.. Inataka kuweka ktk bahasha na kumpa mhusika au kulipa kwa njia nyngne mtakayokubaliana kama kwa benk, n.k
Kwa upande wa cash nadhani kuna sheria kiasi fulani lazima uwe na police escort; kama anataka ulipe cash basi agharamikie police escort wakati wa kuchukua benki, kupeleka site na kurudisha kiasi kilichobaki. Vile vile lazima akukatie bima inahusiana na kubebana na cashWakuu bosi wangu anataka kuniweka matatani kwa kunibebesha fedha kiasi kikubwa kupelekea wafanyakazi mishahara site sasa tumekaa na nimeona ananiweka kwenye risk kubwa ya kuvamiwa na kuibiwa au kupoteza uhai
wanasheria nisaidieni kifungu cha sheria kinachombana mwajiri kulipa mfanyakazi mshahara kupitia benki ili nikiweke hapa kwenye barua ya kumlazimisha kutoka kwa wafanyakazi walio hapa site
Wanasheria na Ma HR msaada wenu
Sent using Jamii Forums mobile app
Employment and labour relation act 2004/ Sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 tukija kifungu cha 28 , (b) malipo ya mshahara yatalipwa eneo la kazi italipwa kwa CASH au kama kutakuwa na makubaliano mengine baina ya muajiri na waajiriwa sasa basi kupitia hayo makubaliano wafanyakazi wawe wameandika maridhiano yao ya kutaka mishahara yao ipitie kwa njia ya bank ila sasa hapo changamoto itakuwa moja boss atakubari mfano sasa nani atabebe zile bank charges za kufanya transfer ya ile mishahara maana yake wafanyakazi wakubali ilo huwa sio gharama kubwa kwa DTB huwa shilingi 100 kila transfer ya mshahara ila tu endapo muajiri atakuwa na account DTB hivyo watakuwa wanahamisha kirahisi au angalieni muajiri wenu ana account gani ili mfungue huko
NOTE Usije ukakubaliana makato na boss wako ya gharama za kufanya transfer ya malipo kabla ya makubaliano na wafanyakazi utakuwa unavunja kifungu cha 28 cha sheria ya kazi na mahusiano kazini mwaka 2004 inachotaka makato yoyote kuwe na makubaliano ya pande 2 au iwe ni yale ya kisheria kama PAYEE yani Kodi na NSSF
Cha mwisho kwakuwa hii sio lazima ni ombi tumia kuomba busara zake maana yake na yeye akisimamia vifungu hamuwezi fika
[/QUO