Kimsingi ssheria ya AML ya Tanzania na nchi zingine za Afrika ililenga kudhibiti fedha haramu kutoka kwa wauza mihadarati, usafirishaji wa binadamu, silaha na mafuta ya magendo ambao huwapa magaidi kama akina Alqaeda na Alshabaab.
Sheria hii Ni ya mwaka 2006 kufuatia mashambulizi ya Osama Bin Laden ya WTC pale New York mwaka 2001. Hivyo basi nchi zote wanachama wa UN walipewa kama TEMPLATE waichukue na wafanye CUSTOMIZATION kwenye nchi zao ili kudhibiti shughuli za UGAIDI.
Lakini nchi za Kiafrika hazikufanya homework ya kutosha kwa kuwa Sheria Ina hoji kila fedha ambayo mtu amepata tofauti na kipato chake kilichozoeleka.
Siku zote watunga Sheria au sera au kanuni huwa wanadhani wanawatungia WAKOSEFU Sheria za kuwabana, wanasahau kuwa nao iko siku watakuwa nje nao watakuja banwa na Sheria hizo hizo.
Kwa mfano kwenye Sheria hii kuna Lecturer mmoja wa UDSM (Dr Ringo Tenga) wa kitivo cha Sheria alihusika kuipitisha kwa kutoa maoni mwaka 2006 akiwa Mkuu wa kitivo na think tank wa Sheria nchini. Akaipitisha kuwa ni NZURI
Lakini mwaka 2017 alishikiliwa kwa Sheria hii hii ya AML ya mwaka 2006 kwa makosa ya kukwepa kodi kwenye kampuni ya mawasiliano ambayo yeye ni mwana hisa. Hapo sasa akiwa Rumande ya Keko ndipo akaanza KULALAMIKA kuwa Sheria haiko vizuri na inakiuka haki za kikatiba.
Huo ndiyo UJINGA wa waafrika