Wanasheria naomba ufafanuzi,kuhusu bunge,spika,jina pendekezwa la waziri mkuu

Wanasheria naomba ufafanuzi,kuhusu bunge,spika,jina pendekezwa la waziri mkuu

boyayoparuparu

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
343
Reaction score
81
Jina la waziri mkuu litakalo pendekezwa kesho ndani bunge,linaweza kuthibitishwa na wabunge wa upande mmoja wa muungano na ikawa ni halali?bunge lenyewe linaweza kuanza vikao vyake bila wabunge wa zanzibar? Spika nae ni halali kuchaguliwa bila wabunge wa zanzibar? Msaada tafadhali
 
Serikali ya ccm imeshasema mambo ya Zanzibar hayatuhusu,, Zanzibar ni sawa na Somalia matatizo yao hayatuhusu
 
Ccm wanadharau wazanzibar kiasi cha kuudhi.nawashukuru wazanzibar kuikataa ccm.msikubali kupuuzwa kiasi hicho.
 
Nadhani mambo mawili yatatokea:
Kama Dr Shein ataingia bungeni kama rais wa Zenj basi wabunge wa Zenj waliokuwemo bunge la 10 nao waje kujichukulia posho zao.
Kama Dr Shein asipoingia, basi litakuwa bunge la bara wala si la Muungano. Na akiingia peke yake, ina maana kakaribishwa tu ka rais mwinginewe yeyote kuja kusikiliza.
Kabla ya kukimbilia kuzindua bunge, JPM kama rais wa JMT angemalizana na Zenj. Lakini kwa kuwa ni ccm inaongoza, huu ni upepo tu kule Zenj hakutuhusu hata kidogo
 
Wabunge wa Zanzibar ni wabunge waliochaguliwa kwa taratibu za Nec, uchaguzi uliofutwa ni wa Zec hivyo wabunge wa znz wapo kama kawaida na wanaapishwa na kuendelea na ubunge kama kawaida labda kama wa CUF watasusa.
Wabunge wakifikia akidi ya theluthi mbili wanaruhusiwa kuendela na utaratibu wa kuthibitisha/kutothibitisha jina la Waziri Mkuu.
Jambo linalo nitatiza ni kuhusu siku alizotumia Magufuli kumtangaza Waziri Mkuu. Sheria inamtaka amtangaze ndani ya Siku 7 tangu kuanza rasmi kazi za Urais(Kuapishwa) sasa hili la kutumia siku 14 sijaelewa mwenye uelewa wa kisheria anijuze!!
 
Ukisoma Ibara ya 51 ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania aya ya pili inampa madaraka Rais kumteua Waziri Mkuu katika muda usiozidi siku kumi na nne(14) tangu aapishwe

"51.-(1) Kutakuwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muunganoatakayeteuliwa na Rais kwa kufuata masharti ya ibara hii naambaye kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Raiskwa kiapo kinachohusika na kiti cha Waziri Mkuu kitakachowekwana Bunge.

(2) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku kumi na nne, baada ya kushika madaraka yake, Rais atamteua Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la Uchaguzi anayetokana na chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi Bungeni au kama hakuna chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi, anayeelekea kuungwa mkono na Wabunge waliowengi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, naye hatashika madaraka hayo mpaka kwanza uteuzi wake uwe umethibitishwa na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za Wabunge walio wengi. "

http://www.tanzania.go.tz/egov_uplo... JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA.pdf
 
Tumeshaambiwa suala la zanzibar linahitaji busara na hivyo sheria imewekwa kwapani hapa ni busara tu.

Kwa hakika kuna mgongano wa kikatiba katika hili suala. Wengi wanakimbila katika ibara ambazo si sahihi na zisizo na tatizo,

kwangu mimi naona ibara ya 66 inayozungumzia composition ya bunge hii ndiyo ina mashiko zaidi, hao wawakilishi watano wa baraza la wawakilishi sijui watatoka wapi? Na kama hawatakuwepo sina hakika kama bunge litakuwa legally composed. Nawaza tu
 
Jina la waziri mkuu litakalo pendekezwa kesho ndani bunge,linaweza kuthibitishwa na wabunge wa upande mmoja wa muungano na ikawa ni halali?bunge lenyewe linaweza kuanza vikao vyake bila wabunge wa zanzibar? Spika nae ni halali kuchaguliwa bila wabunge wa zanzibar? Msaada tafadhali

Kwa mujibu wa katiba ya JMT, IBARA 51. Hao uliowataja wanachaguliwa ama kuthibitishwa na wabunge waliowengi. Msisitizo hapa ni IDADI (MAJORITY)

Hii ni tofauti na kwamfano kura za mabadiliko ya katiba ambayo inataka wingi wa kura kwa uwiano wa Zanj na Tanganyika. Msisitizo ni UWIANANO (PROPOTIONALITY)
 
Back
Top Bottom