Wanasheria nisaidieni

Wanasheria nisaidieni

MAKASSY

Member
Joined
Jan 16, 2013
Posts
95
Reaction score
26
....Kuna bwana mmoja kanunua shamba jirani yetu!mipaka iliyokuwepo tangu awali sikuwahi kusikia tatizo la mipaka.baba yangu alifariki july,ss huyo jirani mama yake ambaye alikuwa mmiliki alishafariki!mtoto wa huyo mama ameuza hilo eneo na kudai mpaka umepinda na kuchukua jukumu la kuweka mipaka mipya.kuna miti ilikuwa upande wa eneo letu amesema iko upande wake!nishaurini
 
Je kuna ramani ya hili shamba (registered land survey)?

Kama hakuna ramani kulikuwa na mashahidi (mjumbe wa nyumba kumi, mzee wa kijiji, nk.) wanaoweza kuapa kortini kuhusu huu mpaka? Ni muhimu hawa mashahidi wafahamishwe maana ya kiapo na adhabu yake watakapo gundulika wamedanganya - perjury.

Kama hivi vitu havipo basi naomba mkae kama majirani na kukubaliana mipaka mipya ni ipi. Lakini baada to ya mipaka mipya kukubaliana tafadhali sana tengeneza ramani ya hili eneo. Siku hizi land survey ni bei poa sana hasa ukizingatia uwepo wa hizi GPS-based tools.

Pole sana.
 
Eneo letu halijauzwa!lililouzwa ni eneo la jirani.eneo letu baba alivunja msitu enzi hizo.ni kijijini na tatizo ni kwamba dosari hii imejitokeza majuzi tu!na nikipindi kirefu sikuwahi kusikia tatizo lolote
 
Sisi tunaishi hapohapo.ni kijijini.hakuna hiyo land survey!tatizo ni kwamba huyo bwana alieuza shamba hilo ni mtoto na mwenye shamba ni wazazi wake na walishafariki nami pia baba yangu alishafariki!
 
Back
Top Bottom