Je kuna ramani ya hili shamba (registered land survey)?
Kama hakuna ramani kulikuwa na mashahidi (mjumbe wa nyumba kumi, mzee wa kijiji, nk.) wanaoweza kuapa kortini kuhusu huu mpaka? Ni muhimu hawa mashahidi wafahamishwe maana ya kiapo na adhabu yake watakapo gundulika wamedanganya - perjury.
Kama hivi vitu havipo basi naomba mkae kama majirani na kukubaliana mipaka mipya ni ipi. Lakini baada to ya mipaka mipya kukubaliana tafadhali sana tengeneza ramani ya hili eneo. Siku hizi land survey ni bei poa sana hasa ukizingatia uwepo wa hizi GPS-based tools.
Pole sana.