Wanasheria pitieni hapa msaada unaitajika

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2014
Posts
4,664
Reaction score
9,929
Poleni na majukumu ya kila siku

Nilikuwa naomba kujua endapo mshitakiwa, kapelekwa kituoni akapata dhamana akatoka, siku ya kesi mshitakiwa uyu kaenda mahakamani anambia inaitajika arudi mahabusu kwani dhamana haipo kwani hakimu anayesikiliza kesi yake hayupo mshitakiwa uyu anachukuliwa na kurudi Mahabusu anapangiwa siku ya kesi, siku ya kesi mshitakiwa anaenda mahakamani anakuta hakimu hayupo hivyo dhamana haiwezi tolewa mshitakiwa anarudi tena mahabusu anapangiwa siku nyingine ya kesi siku inafika anakuta tena hakimu hayupo hivyo hawezi pata dhamana

Sasa naomba muongozo sheria inasemaje hali hii ikijitokeza kwani mshakiwa dhamana Yake ipo wazi tatizo hakimu hayupo hivyo anakosa je kipi kinaitajika kifanyike hata kama hakimu Anayesikilizà hii kesi akiwa ayupo mshitakiwa apate dhamana

Naomba msaada wenu watalaam
 
.

Mkuu, ni wazi kuwa kuna makosa yanayodhaminika katika vituo vya polisi na makosa yanayodhaminika kwa idhini ya mahakama pekee. kwa scenario hiyo kosa hilo dhamana yake inahitaji mahakama kuidhinisha. Mwendesha mashtaka (au polisi kwa mazingira mengine) anayo mamlaka ya kuzuia mtuhumiwa asipate dhamana mpaka pale mahakama itakaposikiliza maombi ya kuomba dhamana. Hii inakuwa na sababu zake, mfano pale mtuhumiwa anapokuwa ni hatari kwa usalama wa raia na mali zao, au pale usalama wake unapokuwa uko hatarini pindi atakapokuwa uraiani. Pia kama hakuna order (amri) ya mahakama kuhusiana ma uhuru wa mshtakiwa (uhuru wa dhamana) mwendesha mashtaka au polisi wana uwezo wa kumsweka mtuhumiwa korokoroni hata kama awali alikuwa uraiani. Pia Mahakama inauwezo wa kutoa amri ya kutiwa ndani (korokoroni/rumande) mtuhumiwa yeyote, kutokana na mazingira na sababu itakayotoa.

Dhamana inakuwa wazi kwa kila kosa linalodhaminika. Kutokuwepo kwa hakimu hakuondoi haki ya mtuhumiwa/ mshtakiwa kupata dhamana. kwa maneno mengine mazingira ya kimahama, kama vile kutokuwepo hakimu/jaji hayatumiwi na hayatakiwi kutumika kama silaha ya kudhulumu haki ya msingi ya mtuhumiwa. Maombi ya dhamana husikilizwa na afisa (hakimu/jaji) yeyote aliyepo kituo cha kazi, hayana uhitaji wa kusubiri presiding judge/magistrate kama ilivyo kwenye trial.
Inapotokea hakimu au jaji anayehusika na kesi tajwa hayupo katika kituo cha kazi, basi hakimu au jaji yeyote aliepo kituoni hapo anakuwa na mamlaka ya kusikiliza maombi ya dhamana. (hapa kuna tofauti ya kuutaratibu (procedure) kama mtuhumiwa atakuwa alikiuka masharti ya dhamana iliyokwishatolewa awali, na anataka kuomba dhamana kwa mara nyingine)

Kwa ufupi, mshtakiwa (au wakili wake) anaweza kupeleka maombi ya dhamana kwa hakimu yeyete mwenye mamlaka aliyepo kwenye mahakama ambayo kesi ya mtuhumiwa inatajwa.
 
Shukrani kiongozi kwa ufafanuzi mzuri naomba tena kujua endapo hayo yana tendeka yapaswa niende kutoa tarifa wapi kwa msaada zaidi
 
Shukrani kiongozi kwa ufafanuzi mzuri naomba tena kujua endapo hayo yana tendeka yapaswa niende kutoa tarifa wapi kwa msaada zaidi
Kiongozi, sehemu muafaka ya kutoa taarifa kama unaona hayo yanatandeka ni kwa hakimu mfawidhi kama ni mahakama za mahakimu. Kama ni mahakama kuu muone msajili (District Registrar). Hakimu mfawidhi, ambaye ndiye haswa anahusika kugawa mafaili ya kesi kwa mahakimu wengine, anaweza kumpangia hakimu mwinginie hiyo kesi, au kujipangia mwenyewa akasikiliza maombi yenu.
 
Mkuu Dragoon umesema vyema. Lakini, naomba niongeze kidogo. Kwanza, dhamana hutolewa na mahakama hata kama mshtakiwa alipewa dhamana na polisi. Jambo ambalo hufanywa kimakosa na walio wengi ni kutoomba dhamana mahakamani wakati wa shauri. Yaani, mshtakiwa anasubiri Mhe. Hakimu au Mwendesha Mashtaka aseme kuhusu dhamana.

Pili, dhamana, kwa kesi iliyokwishapangiwa Mhe. Hakimu, hutolewa na Hakimu husika tu. Kikubwa ni kujitokeza mbele ya Hakimu husika na kuomba dhamana. Dhamana haiwezi kutolewa na Hakimu asiyehusika na kesi husika. Ndiyo maana hushauri washtakiwa kujitahidi kuwa na Mawakili Wasomi ambao, pamoja na mambo mengine, hujua la kufanya kwa wakati na kwa usahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…