Wanasheria tunaomba mtusaide hapa

Wanasheria tunaomba mtusaide hapa

bne

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2016
Posts
1,679
Reaction score
2,016
Ni kwa jinsi gani watu hawa wafuatao wanavyoweza kupata haki zao kutokana na maamuzi ya kukurupuka ya serikali hii'Tangu serikali ilivyoamua kubadilisha sifa za kujiunga chuo kikuu kupitia TCU maelfu ya watanzani wamekosa nafasi hizo za kujiendeleza kimasomo.

Kumbkeni kuwa sera ya zamani ya elimu na ambayo ilidumu kwa muda mrefu ilikuwa inamruhusu yeyote mwenye (two principle) yaani kuanzia pointi 2 za kidato cha nne alikua anaruhusiwa kabisa kupata elimu yake ya chuo kikuu, na hii ilikua ni sera ya serikali katika elimu hivyo watu wote walisoma kwa mtizamo na mlengo huo.

Sasa inapokuja ghafla serikali hiyohiyo inabadilisha sera yake ghafla hata bila ya kuwaandaa wananchi wake kuhusu mabadiliko ya sera hiyo na kupelekea maelfu ya ya watanzania kuathirika, Je sheri haiwezi kutumika ili kwaokoa watanzania hawa?

Sababu kinachotia shaka ni kwamba, sera hii mpya inamathiri hata yule aliyesoma siku za nyuma wakati wa sera za pointi 2, na mbaya zaidi hata serikali haikuweza kutoa ilani kuwa labda kuanzia mwaka fulani wa masomo kutakua na mabadiliko ya kisera, bali ilichofanya ni ukatili wa mabavu uliosema kuwa kuanzia sasa kuna mabadiliko haya,Je hiyo ni haki?

Mwanasheri mmoja kutoka nchi jirani aliniambia kuwa shida ya watanzania ni kutokujua kudai haki zao, yakwamba sisi hukubali kila kitu hata kama tunaonewa lkn akasema kama mtadai haki hiyo nakuonyesha mahakamani kwa jinsi mlivyo athirika uwezekano mkubwa wa kushinda upo.

Sio siri vijana wetu wengi pamoja na wafanyakazi wengi waliotaka kujiendeleza wameathirika vibaya, hata kama kulikua na umhimu wa kubadili sera hiyo basi serikali ingetoa muda mf,kuazia mwaka wa masomo 2017 lkn hiki kilichofanyika hakikubaliki hata kidogo.

Natoa wito kwa wanasheria wetu huu ndio wakati wakusimama imara kuwatetea watanzania ikichukuliwa maanani kuwa wanzania wengi hawajui sheria na haki zao,na ni masikini wenye uchumi dhaifu. Msipowasaidia ninyi basi serikali hii itawaumiza.

Na sisi watanzania tutakua tayari kushilikiana nanyi.

NAWAKILISHA.
 
Malizeni kesi haraka kuna trilioni mbili nitawagawia!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kweli kabisa WATANZANIA HAWAJUI HAKI ZAO. Tena watu wanaofanya kazi serikali wanafikiri kwamba raia bado ni watumwa wanaolazimishwa kuvumilia tu.
 
  • Thanks
Reactions: bne
Kweli kabisa WATANZANIA HAWAJUI HAKI ZAO. Tena watu wanaofanya kazi serikali wanafikiri kwamba raia bado ni watumwa wanaolazimishwa kuvumilia tu.
Umesema kweli MKUU hebu tujalibu kuwaamsha wanasheria wetu wawe wa naona maeneo ya kusaidia wanyonge kama ktk sakata hili.
 
Back
Top Bottom