Wanasheria wa Diddy wamepeleka ombi nyingine la dhamana la mteja wao

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Timu ya wanasheria wa Gwiji wa miondoko ya Hip-hop Ulimwenguni ‘Sean Combs’ a.k.a ‘Diddy’ imewasilisha rufaa ya tatu ya kuachiliwa kabla ya kusikilizwa kwa kesi zinazomkabili katika Mahakama ya Rufaa ya Marekani baada ya majaribio ya awali kukataliwa.

Rufaa hiyo inapinga uamuzi uliotolewa na Wilaya ya Kusini ya New York wa kumnyima dhamana mara mbili rapper huyo, ukidai kuwa anaweza kuwatisha mashahidi na kucheza mchezo mchafu ili haki isitendeke kwa wanaomshitaki kutokana na utajiri wake au anaweza kukimbia kabisa.

Timu ya ‘Diddy’ inaomba kuachiliwa kwake mara moja kwa masharti yanayofaa ya dhamana, baada ya Mwanzilishi huyo wa Bad Boy Records, kukamatwa mwezi uliopita kwa madai ya Kula njama za mauaji, biashara ya ngono kwa nguvu na ulaghai.

Hata hivyo Gwiji huyo wa Hiphop, alikana hatia na anaendelea kuzuiliwa katika Gereza la Metropolitan Detention Center huko Brooklyn, akisubiri kesi yake kuamriwa.

Soma Pia:
Hata hivo ‘Diddy’ alikuwa tayari kulipa hadi dola milioni 50 kama bondi sawa na fedha za Kitanzania zaidi ya Bilioni 136, na kutoa dhamana ya nyumba yake ya Miami yenye thamani ya dola milioni 48 sawa na fedha za Kitanzania zaidi ya Bilioni 130 pamoja na nyumba ya mama yake.
 
Hakuna kuachiwa huyo Mwamba aendelee kukaa Jela wakati kesi yake ikiendelea ,ukizingatia kwa USA hana hata 100 ,akiachiwa anaweza kukimbia nchi na kwenda sehemu nyingine kama alivyowakimbia Feds mwanzoni.
 
Timu ya wanasheria wa Gwiji wa miondoko ya Hip-hop Ulimwenguni ‘Sean Combs’ a.k.a ‘Diddy’ imewasilisha rufaa ya tatu ya kuachiliwa kabla ya kusikilizwa kwa kesi zinazomkabili katika Mahakama ya Rufaa ya Marekani baada ya majaribio ya awali kukataliwa.

Rufaa hiyo inapinga uamuzi uliotolewa na Wilaya ya Kusini ya New York wa kumnyima dhamana mara mbili rapper huyo, ukidai kuwa anaweza kuwatisha mashahidi na kucheza mchezo mchafu ili haki isitendeke kwa wanaomshitaki kutokana na utajiri wake au anaweza kukimbia kabisa.

Timu ya ‘Diddy’ inaomba kuachiliwa kwake mara moja kwa masharti yanayofaa ya dhamana, baada ya Mwanzilishi huyo wa Bad Boy Records, kukamatwa mwezi uliopita kwa madai ya Kula njama za mauaji, biashara ya ngono kwa nguvu na ulaghai.

Hata hivyo Gwiji huyo wa Hiphop, alikana hatia na anaendelea kuzuiliwa katika Gereza la Metropolitan Detention Center huko Brooklyn, akisubiri kesi yake kuamriwa.

Soma Pia:
Hata hivo ‘Diddy’ alikuwa tayari kulipa hadi dola milioni 50 kama bondi sawa na fedha za Kitanzania zaidi ya Bilioni 136, na kutoa dhamana ya nyumba yake ya Miami yenye thamani ya dola milioni 48 sawa na fedha za Kitanzania zaidi ya Bilioni 130 pamoja na nyumba ya mama yake.
Firauni asipewe dhamana
 
Back
Top Bottom