Wanasheria wa serikali: Ni hujuma au hamjui kazi yenu??

Wanasheria wa serikali: Ni hujuma au hamjui kazi yenu??

SirBonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2010
Posts
378
Reaction score
435
Napata shida shida sana kuelewa kwamba inakuwaje serikali inapoteza kesi nyingi sana ambazo inafungua na kusimamiwa na wanasheria wake? Achilia mbali hizi za kifisadi angalia kesi za akina Zombe, Mungai na sasa Mwakalebela!
Sisemi kwamba nataka hawa jamaa wafungwe, la hasha! issue ni kwamba kesi hizi (mfano ya Mungai na Mwakalebela) eti zimefutwa kwa sababu kuna vipengele vya sheria havikufuatwa wakati wa kufungua kesi..Haiingii akilini, ni vipengele gani ambavyo wanasheria binafsi wanavijua lakini nyinyi wa serikali hamvijui?? Hii ni aibu kubwa kwenye tasnia nzima ya sheria!
Sijui wadau wengine mnalionaje hili...Mi nahisi ni hujuma inaofanywa na hawa watu!
Naomba kuwasilisha...
 
Mkubwa umenena kweli hilo tatizo kubwa na lisipo angaliwa vyema linaweza kuleta sura mpya.
 
Tatizo unasahau kuwa hata hao wanao ishinda serikali wamesomea tanzania na hapo zamani walikuwa wanasheria wa serikali, hoja ya msingi ni yupi anajiandaa kwa makini kumtetea mwenzake kwa hoja!
 
Usiseme wanasheria wa serikali sema wanasheria wa PCCB. Pia ujue kesi nyingi za aina hiyo zimefunguliwa kisiasa zaidi ya kisheri.
 
Back
Top Bottom