Wanasheria wetu naomba kujua kazi zenu kwa jamii

mwembemdogo

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2016
Posts
2,282
Reaction score
1,252
Watanzania tumekuwa tunakabiliwa na matatizo mengi kimaisha, kimwili na kisheria lakini ya kisheria tunashindwa kujua kama ni sehemu ya kazi zenu hebu mtujuze kazi zenu.
 
lete matatizo yako lipia kuongea nasi utajua kazi zetu kwa sababu sheria haziruhusu kujitangaza kazi zetu na isitoshe vyote uvionavyo ni kazi za sheria hakuna sheria hakuna maisha
 
Una sh ngapi?
Umesahau madaktari walipogoma mlivyowasema na kufurahia Ulimboka ashugulikiwe.
Wanasheria kaeni kimya.
Hata hiyo kesho najua hakuna sapoti.
Ngoja tuisome namba wote akili ikae sawa tujue tofauti ya kudai na kubembeleza haki.
 
lete matatizo yako lipia kuongea nasi utajua kazi zetu kwa sababu sheria haziruhusu kujitangaza kazi zetu na isitoshe vyote uvionavyo ni kazi za sheria hakuna sheria hakuna maisha
Wanasheria wetu wamekuwa kama madalali wanangoja mtu auze nyumba au gari wapate dili hakuna cha zaidi kwenye jamii. Uliona wapi mwanasheria sheria za nchi zinavunjwa kwa makusudi na wenyewe wanakaa kimya. haki za raia zinaporwa wenyewe wako kimya. Wanasheria wetu tofauti na wanasheria wa nchi kama Kenya ambao wako tayari kufungua kesi dhidi ya jamhuri kama wakiona sheria iliyotungwa na serikali inakwenda kinyume na Katiba ya nchi. Hapa kwetu hiyo kazi aliachiwa Hayati Mtikila na baada ya kufa hata utekelezaji wa hukumu yake hakuna wa kuisimamia dhidi ya Mgombea binafsi. Wanasheria wetu wanangoja watu wagombane aende kumshawishi mmoja wao namna ya kudai fidia ili afungue kesi yeye apige hela. hawajali mambo ya jamii na wala hawajui kama ni sehemu ya majukumu yao. Umesikia anauliza unashida gani? maana anauliza kuna dili gani?
 
Shyster lawyers!
 
Huo ndio ukweli wenyewe.
 
Aibu juu yao weng wana pelekwa pelekwa na kile INA itwa mamlaka ya juu na wenye pesa zao tuu mnyonge afie mbal
 
UHALISIA WA TAALUMA YA SHERIA NA UDAKTARI.
huwezi kwenda kwao mpaka uwe na matatizo yenye mgongano wa kisheria au kiafya(matatizo hayo)
huwezi onana nao kama huna pesa (yaani una matatizo alafu unatakiwa utoe pesa)
wengi wao wamesahau kuwa uwepo wao ni kwa ajili ya kuimarisha jamii husika
Cha ajabu sasa hadi madaktari wamekuwa mstari wa mbele kudai rushwa hata kama mgonjwa ni hoi hae,Wanasheria hawaexercise their professional for the well being of the SOCIETY
Wanasheria wa nchi yetu pamoja na kuijua sheria lakini bado hawako huru,TAIFA GANI HILI?
kila siku utamsikia Tundu Lissu kuwa amewashinda wanasheria wa serikali,je hawa wa serikali hawana utashi na taaluma yao? Ni nani aliyewateua kudharirisha Jamhuri kwa kiwango cha juu kiasi hiki?.
But they have been so busy misleading the Law mfano huyu CAG alipohojiwa hapo juzi alionekana kukubaliana na agizo la kukataza mikutano ya kisiasa hali ya kuwa swala hilo ni kinyume na sheria za vyama vya siasa nchini,mfano mwingine nakumbuka hata yule Dk.Tulia alihusika kupindisha sheria juu ya swala la MITA MIA MBILI KULINDA KURA MWAKA JANA,hivyo basi wanasheria wetu WANAPINDISHA SHERIA KULINDA TEUZI ZAO.
SIO KAMA HAWAWEZI KULIPINGA HILO,SIO KAMA HAWANA POWER HIYO KAMA PROFESSIONALS,NA SIO KAMA WAMEKATAZA KIKATIBA ILA HAWATAKI KUITETEA KATIBA YA NCHI YETU.
[HASHTAG]#kesi[/HASHTAG] ikiendeshwa kwa kiingireza CAG HACHOMOKI HATA KIDOGO.
TUMESHUHUDIA KULE ARUSHA MAWAKILI MPAKA WA SERIKALI WAKIANDAMANA BAADA YA WAKILI MWENZAO KUBAMBIKIWA KESI AKIWA KITUO CHA POLISI WALIVYOREACT,TANZANIA NZIMA ILIJUA HILO.
Je vipi leo hii hushindwe kulitetea taifa kwa kukiukwa misingi ya kikatiba au kwa kuwa mkuu wa kaya ndiye aliyekutea CAG?
 
Maneno mazito kweli mtikila tu ndie alieweza....
 
Mtawaonea tu wanasheria bure,
>>kazi ya uanasheria si lelemama kama wengi wafikiriavyo, inahitaji moyo mgumu na commitment,
>>wengi wamesomeshwa na fedha za wazazi wao (hakuna mtu anayesoma bure Tz)
>>mtu anatumia gharama nyingi sana na muda mwingi mpaka kuja kuwa mwanasheria,
>>kuendesha kesi ni gharama pia na muda unatumika pia kuandaa hiyo kesi
>>mwanasheria ni mtu kama watu wengine mwenye majukumu kama yako
>>mwanasheria analipa kodi kama mfanyabiashara mwingine, ana TIN na Business License
>>analipia leseni ya uendeshaji wa huduma zake (practising license) kila mwaka
>>analipia huduma nyingine za kuendesha ofisi yake na wafanyakazi
>>wakati mwingine anakutana na kesi ambayo inaweza hatarisha amani ya maisha yake
>>kazi ya uanasheria siyo ya lazima kutoa huduma kwa jamii bure
>>Tanganyika Law Society inatoa msaada (Pro bono) kwa watu ambao hawana uwezo wa kifedha kwa kuwapa mawakili

kwahiyo mtu unapokuja hapa na kuanza kutoa lawama kana kwamba hii hudumu ni ya bure fikiria kwanza hayo hapo juu, yaani ni sawa uende dukani kwa mtu akupe huduma bure wakati yeye ameigharamia, pamoja na kwamba wanasheria wanatoa huduma mbalimbali bure (msaada wa sheria) kupitia vituo mbalimbali nchini na vipo vingi sana kila wilaya pamoja na kujitangaza kwenye vyombo mbalimbali vya habari, na kwenye mitandao ya kijamii, ni watu wachache sana wanaothubutu kwenda kuomba msaada wa sheria bure.
sasa najiuliza mlitaka wanasheria wawafate nyumbani kwenu mkiwa na matatizo ya kisheria wawasaidie?, au watembelee sehemu zenye migogoro ya ardhi ndo wawasaidie kutatua?, matatizo ya kikaktiba ni mengi sana yametatuliwa na wanasheria hata juzi tumeona la wakili Jebra Kambole khs ndoa za utotoni, suala la Mtikila lilikuwa ni personal interest wala si public interest, yeye alikuwa na masilahi yake binafsi so huwezisema eti hakuna watu ambao wanantetea katiba ama wananchi, kumekuwa na vipindi vingi sana kwenye vyombo vya habari kwa ajili ya kutoa elimu ya sheria, (tatizo hamfuatilii)
waTanzania mnataka hata katiba mje mfundishwe majumbani kwenu, na bado mmekuwa wabishi sana, hao hao wanasheria wakitaka kuwaelimisha pamoja na kutoa vielelezo ninyi ndo mnageuka kuwa wanasheria, humu jamii forums, pamoja na kejeli mnazotoa kwa wanasheria, lakini bado misaada ya kisheria inatolewa.

kumbukeni msaada wa sheria ni hiari ya mtu, sheria ni kazi kama kazi nyingine, ukitaka msaada nenda kamuone wakili ofisini kwake, lipa ada, uone kama hujapewa huduma.

halafu huduma ya sheria haitangazwi.
 
ID yako inajieleza vizuri
 
Maelezo yako yanaonesha utofauti mkubwa wa kiutendaji wa wanasheria wetu na wanasheria wa nchi nyingine. Kusomeshwa na wazazi wako hakukufanyi uwe isolated na jamii. Kesi ya Mtikila haikuwa ya Binafsi na wala si kwa interest yake. Hujui kuwa yeye alikuwa na chama tayari ambacho kilikuwa kinampa uwezo wa kugombea urais? sasa ubinafsi wa kesi yake uko wapi? Ile kesi ni ya kikatiba kwani katiba inasema kila mtu ana haki ya kuchagua au kuchaguliwa so hakuna kesi binafsi hapo.
 
sawa, kesi ya mtikila ilikuwa ni ya kikatiba, lakini kilichompeleka mahakamani ilikuwa ni personal interest, kwani ni mambo mangapi aliyafanya kuwatetea wananchi?
mtu kusomeshwa na mzazi wake ni sawa na mfanyabiashara aliyejitafutia mtaji then unataka atoe bidhaa bure, ingawa wanasheria wanatoa huduma bure, but ninyi mnavyoidai hiyo huduma kana kwamba mliwachangia ada, kwenye profession zenu mmesaidia nini, ma Eng wanasaidia nini bure, wahasibu wanasaidia nini bure, tukitoa hizo huduma bure, maisha yetu, ofisi zetu tutaendeshaje?
 
hahahaha Nimeipenda hiyo statement yako ya Mwisho, ' tukitoa hizo huduma bure, maisha yetu, ofisi zetu tutaendeshaje?'. Umejificha weee mwisho ukajitambulisha kwamba kumbe nawe ni Mwanasheria. Nakutakia Kazi njema. Maana fisi alipojibandika pembe ahudhurie sherehe za wanyama wenye pembe alipowekwa juani nta ikayeyuka alishindwa kuvumilia hatimaye akawaambia wenyeji wake tuhame hapa zinayeyuka maana alibandika pembe kwa nta hivyo zilitaka kudondoka. Usiringanishe professional zingine ukashindwa kutimiza wajibu wako kwa jamii mkuu
 
Una sh ngapi?
Umesahau madaktari walipogoma mlivyowasema na kufurahia Ulimboka ashugulikiwe.
Wanasheria kaeni kimya.
Hata hiyo kesho najua hakuna sapoti.
Ngoja tuisome namba wote akili ikae sawa tujue tofauti ya kudai na kubembeleza haki.
Miongoni mwa Kada ninayoidharau humu Duniani ni hao jamaa...wanajifanya watu Special kumbe HOVYO sana! Watu waliotayari kuuza utu wao sababu ya pesa
 
...kuna kitu labda hatujaelewana, watu wanavyolalamika kana kwamba wanasheria wapo kwa ajili ya kutoa huduma bure, ulishawahi ona wapi, nchi gani, (save for legal aid centres) ni lazima ulipie, na ile dhana ya kusema watu wanapindisha sheria sjui huwa mnaitoa wapi.
by the way, mimi nilikuwa sijifichi kwani sijaanza kuzungumzia sheria au kutoa misaada ya kisheria humu leo.
 
Soma vizuri Comment zako tangu mwanzo ulikuwa unatumia third person (Yaani wao) kisha mwisho ndiyo ukatumia first person (Yaani) Mimi). Ndiyo maana nikasema umejificha. Si mbaya nikigombana na mke wangu nitakutafuta uniwakilishe Mahakamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…