Wanasheria wetu naomba kujua kazi zenu kwa jamii

Soma vizuri Comment zako tangu mwanzo ulikuwa unatumia third person (Yaani wao) kisha mwisho ndiyo ukatumia first person (Yaani) Mimi). Ndiyo maana nikasema umejificha. Si mbaya nikigombana na mke wangu nitakutafuta uniwakilishe Mahakamani
...haha, nikweli nilikuwa natumia third person, bt si kwa intention ya kujificha....ukigombana na mke wako utatakiwa uende baraza la usuluhishi wa ndoa (marriage conciliation board) lipo kila wilaya huduma zao ni kama bure tu. teh
 
Moja ya kazi za wanasheria ni kutoa huduma bila malipo yani (legal Aid) as a cooperate Social responsibility mara nyingi ni kwa wale wenye uhitaji maalum na wasio na uwezo wa kifedha.
Sambamba na hilo kuna legal Aid schemes, vituo vinavyotoa msaada wa kisheria bila malipo.
Mfano:-
1.State scheme ambayo huwa kuna wanasheria wanaojitolea na hulipwa na serikali.
2.Tanganyika law society
3.University of Daressalaam legal aid scheme na NGOs kama kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC na nyinginezo.
Nakubaliana nanyi wakuu kwl tumepoteza tunu na pioneer wa utetezi wa haki, late Mtikila alithubutu na athari za aliyoyafanya tunafaidika nayo mpaka hivi leo.
Hata hivyo wanasheria bado wanafanya mambo makubwa na harakati za. Utetezi kwa jamii zipo palepale mfano hivi majuzijuzi tumeshuhudia kesi ya kupinga ndoa za utotoni iliyofunguliwa na dada yetu Rebeca Gyumi mkurugenzi wa msichana initiative...... pia kuna kesi nyingi zinazofunguliwa na watu kama kina Jeremiah Mtobesya moja ya kesi zake imepelekea kupunguzwa kwa madaraka ya DPP madaraka ambayo yalikuwa yakipingana na katiba na kesi nyingine nyngi ambazo kila kukicha zinafunguliwa kwa manufaa ya jamii kwa ujumla.
Lakini mtoa mada ametoa changamoto kwa wanasheria ambayo inatakiwa kupokewa kwa mikono miwili na kuongeza chachu na uwajibikaji wa wanasheria kwa jamii yetu na kwa maendeleo na manufaa ya taifa letu
 
Unaposema huduma ya sheria haitangazwi, ni kwa Tz tu?
 
....sijajua kwa nchi nyingine, but Tz hairuhusiwi kufanya matangazo
Kwann? labda kuna sababu muhimu ya kuwakataza wanasheria wasijitangaze??? Je,nyinyi wanasheria mnalichukuliaje hilo mmeridhia? Na ipo kwenye sheria kwamba hamruhusiwi kufanya matangazo. Bhasi kazi yenu haina uhalali kwann mfanye kwa kificho? Hayo ni maswali yangu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…