#COVID19 Wanasiasa kaeni pembeni katika suala la Corona

MIGNON

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2009
Posts
4,108
Reaction score
5,110
Kama nchi tunaendelea kulumbana kuhusu Covid-19. Hatujapata muafaka bado na tuna makundi mawili makubwa.

Kuna mambo ambayo yanaendelea lakini ni kwa kipindi kifupi na kwa gharama kubwa ya maumivu na mateso kwa watu.
  1. Hakuna kiongozi mkuu ambaye amesimama na kukiri ya kuwa Corona ipo. Wote wanazunguka na kuzungumza kwa "soft tone" as if wanapeleka barua ya posa.
  2. Pamekuwa na ongezeko kubwa la uhamasishaji wa matumizi ya tiba mbadala huku watu wakiibua terminology mpya (mkurugenzi wa NIMR" anasema tiba lishe, kuna wanaosema dawa). Huko Mtwara Mkuu wa mkoa anataka kuandikisha watu wenye uwezo wa kutibu "changamoto za upumuaji.
  3. Naibu waziri wa Afya anashindwa kuwajibu WHO kuhusu takwimu za Corona anaishia katika "kuchakata na ku digest". Huyu ni mwanasayansi ambaye imani yake katika takwimu ina walakini kidogo.
Kama Taifa tuliingia katika kashfa kubwa ya "Babu wa Loliondo" na kwa ukweli ni aibu ambayo itakuja kujadiliwa baadae vizazi vinavyokuja vitakapoondoa uoga tulio nao sisi. Bila aibu tunaingia tena kwenye kashfa nyingine ya kujaribu kulifanya tatizo la kisayansi kuwa ni tatizo la kiimani.Tulionywa kuhusu "second wave" na sasa na tuna starin ingine kali zaidi.
Serikali itusaidie kwa kutueleza haya kwa uwazi kabisa.
  1. Kama kuna corona itamke wazi na kwa sauti inayotakiwa na kusimamia mapambano hayo kwa nguvu zote.
  2. Kama hakuna corona itamke wazi na isimamie watu kujikinga ili isiingie nchini kwetu
Mojawapo kati ya hayo likifanyika tutakuwa tumepiga hatua kubwa kwani kwa sasa kuna waliojitahidi kuweka maji na sabuni lakini wanwaji hakuna. Kuna wanaovaa baroka na kuingia ndani mwendokasi na kukuta katika abiria mia ni watatu waliovaa.
 
Subiria vijana wa mataga na UVCCM wanakuja kukupa majibu mujarabu. Huwa wana swali lao wanalouliza kuwa "Kwenu wamekufa wangapi?
 
yani hii nchi imekuwa ya (ajabu ×2) kweli, kila kitu kinaingizwa kwenye siasa ikiwemo specialization za watu mpaka mambo yasiyohusiana na siasa wanalazimisha iwe siasa, skuiz elimu imekuwa siasa, afya imekuwa siasa, kilimo siasa, biashara siasa, karibia sekta zote siasa
Kama kila kitu ni siasa inabidi wanasiasa wakalime, wakatibu wagonjwa, wakawe walim, nk, maana wanajikuta wanajua kila kitu.
 
Tabu hii nchi haina wazalendo,imejaa wachumia tumbo na njaa njaa waliopata vyeo vya kisiasa kujitatulia shida zao,
Yaani hii nchi ukipata cheo cha kisiasa tu na taaluma zote utaziweza hata ikiwa kupasua ubongo au moyo wa mtu sasa imagine hadi Mh jiwe akajigeuza kiongozi wa kiroho kwa kutangaza maombi ya Siku tatu na hapo hapo akajipa uganga wa kienyeji wa kupiga nyungu we unadhani kama
Nchi tutapiga hatua kweli?
 
Amna korona wala covid ni WHO wanatafuta kiki,halafu sku izi dunia ni kijiji,kila kitu kinagugulika zamia na shahada yako ya uzamivu ndani ya guguli ibuka na taaluma uliyoipata kuhusu corona,usingojee Raisi kila siku akuambie wakati alishasema huko mwanzoni mpaka watu wakamuelewa na ugonjwa ukapunguza kasi.
waTz jiongezeni msisuburi raisi awaongonze kama magombe.
 
Nachofahamu, watu wakiwa kwenye kikao, na kukaweko mada jadidi" kama agenda Hiyo haijapata solution yake, watu wataendelea kuijadili Ili kupatikane solutions yake

Na mpaka huu muda! Hakuna mwenye solution ya Corona na ndiyo Maana kuna wito wa kila mtu kuonyesha utaalamu wake na mwisho wa siku, atakayekuja na jibu ndipo mjadala utafungwa

Wewe Mleta mada na wewe kama unautaalamu wako kuhusu hii mada, Peleka wizara ya Afya na usiwe mtu mwenye wivu pindi wenzako wakiendelea na mchakato huo

Nimegundua kitu kimoja kwenye akili yako, Kumejaaa utumwa na ujinga mwingi Maana huwezi kujiamini na Wala hutaki ujitawale

Kama huna huo uwezo wa kuichakata Hiyo mada kaa kimya Wenye akili wazidi kutumia upeo wao
 
Nachofahamu, watu wakiwa kwenye kikao, na kuwaweko mada jadidi" kama agenda Hiyo haijapata solution yake, watu wataendelea kuijafili Ili kupatikane solutions yake

Na mpaka huu muda! Hakuna mwenye solution ya Corona na ndiyo Maana kuna wito wa kila mtu kuonyesha utaalamu wake na mwisho wa siku, atakayekuja na jibu ndipo mjadala utafungwa

Wewe Mleta mada na wewe kama unautaalamu wako kuhusu hii mada, Peleka wizara ya Afya na usiwe mtu mwenye wivu pindi wenzako wakiendelea na mchakato huo

Nimegundua kitu kimoja kwenye akili yako, Kumejaaa utumwa na ujinga mwingi Maana huwezi kujiamini na Wala hutaki ujitawale

Kama huna huo uwezo wa kuichakata Hiyo mada kaa kimya Wenye akili wazidi kutumia upeo wao
Naona mwana siasa nguli ukitoa povu zito kwa mtoa mada haahaaahaaa
 
Kama nchi tunaendelea kulumbana kuhusu Covid-19. Hatujapata muafaka bado na tuna makundi mawili makubwa.

Kuna mambo ambayo yanaendelea lakini ni kwa kipindi kifupi na kwa gharama kubwa ya maumivu na mateso kwa watu.
  1. Hakuna kiongozi mkuu ambaye amesimama na kukiri ya kuwa Corona ipo. Wote wanazunguka na kuzungumza kwa "soft tone" as if wanapeleka barua ya posa.
  2. Pamekuwa na ongezeko kubwa la uhamasishaji wa matumizi ya tiba mbadala huku watu wakiibua terminology mpya (mkurugenzi wa NIMR" anasema tiba lishe, kuna wanaosema dawa). Huko Mtwara Mkuu wa mkoa anataka kuandikisha watu wenye uwezo wa kutibu "changamoto za upumuaji.
  3. Naibu waziri wa Afya anashindwa kuwajibu WHO kuhusu takwimu za Corona anaishia katika "kuchakata na ku digest". Huyu ni mwanasayansi ambaye imani yake katika takwimu ina walakini kidogo.
Kama Taifa tuliingia katika kashfa kubwa ya "Babu wa Loliondo" na kwa ukweli ni aibu ambayo itakuja kujadiliwa baadae vizazi vinavyokuja vitakapoondoa uoga tulio nao sisi. Bila aibu tunaingia tena kwenye kashfa nyingine ya kujaribu kulifanya tatizo la kisayansi kuwa ni tatizo la kiimani.Tulionywa kuhusu "second wave" na sasa na tuna starin ingine kali zaidi.
Serikali itusaidie kwa kutueleza haya kwa uwazi kabisa.
  1. Kama kuna corona itamke wazi na kwa sauti inayotakiwa na kusimamia mapambano hayo kwa nguvu zote.
  2. Kama hakuna corona itamke wazi na isimamie watu kujikinga ili isiingie nchini kwetu
Mojawapo kati ya hayo likifanyika tutakuwa tumepiga hatua kubwa kwani kwa sasa kuna waliojitahidi kuweka maji na sabuni lakini wanwaji hakuna. Kuna wanaovaa baroka na kuingia ndani mwendokasi na kukuta katika abiria mia ni watatu waliovaa.
Mkuu, mimi napata hisia kuwa watawala kwa makusudi wameamua kulipuuzia janga hili la C-19 kwa kuwa wanataka lienee miongoni mwa watu ili wapate kusahau dhuluma iliyotendeka wakati wa uchaguzi wa 2020.
 
Back
Top Bottom