Mtoa mada, nadhani vyama vingi vya siasa vina lengo na nia moja nalo ni katiba mpya. Lakini chama kimoja tu ndiyo kikwazo nacho ni CCM. Napenda nikuthibitishie usemi wangu kwa vigezo vifuatavyo: Kwanza ni kwanini muswada wa katiba mpya ujadiliwe kwenye miji mitatu ya Zanzibar, Dodoma na Dar? Pili ni kwanini muswada uandaliwe kwa lugha ya kigeni kama kweli lengo ni kutaka kuwahusisha watanzania wote. Tatu ni kwanini mijadala ifanyike kwenye sehemu zenye nafasi finyu?