Wanasiasa mnaojihusisha na udhamini wa mchezo wa mpira huku mtaani tunaomba msiwaache vijana baada ya kupata mnachokitafuta kwao

Wanasiasa mnaojihusisha na udhamini wa mchezo wa mpira huku mtaani tunaomba msiwaache vijana baada ya kupata mnachokitafuta kwao

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Kuelekea uchaguzi wa mwaka elfu mbili na ishirini na tano (2025) Kila ninapopita mtaani naona vijana wamependeza na jezi zenye maandishi ya DIWANI CUP, MBUNGE CUP, JIMBO CUP nk.

Vijana wanafanya mazoezi kwa MORALI Tena wanasema mh fulani ameahidi kuwapambania vijana mpaka watakapo timiza ndoto zao.

NALIA NGWENA naona ni Jambo jema kabisa lakini wasiwasi wangu ni kuwa vijana wasije kutumika Kama ngazi halafu watelekezwe/watupwe kwenye bin Kama kondomu iliyokwisha tumika.

Chonde chonde wanasiasa msiwaache vijana Hawa mnaopasha nao misuli Kila asubuhi na jioni nakuonesha Nia ya dhati kuwa mpo nao bega kwa bega nakuwaahidi kuwa mtahakikisha mnakuza vipaji vyao.
 
Mbona kama umeandika kimafumbo kuwa Utopolo hisiachwe na wanasiasa mpaka imalizie mechi kule Algeria.
 
Back
Top Bottom