are we looking for an angel?
definitely not!
Kuhusu Mrema kinachonipa shida ni kusema yeye ndiye aliyepata kura nyingi za wapinzani kuliko mwingine yeyote , tangu 1995 mpaka 2005 hakuna mwingine upinzani aliyepata kura nyingi kama mrema! then kuanzia sijui lini ikajulikana ni pandikizi la CCM, swala ni je 1995 alikuwa pandikizi au issue za pandikizi zimekuja baadae?
I have different opinion here; hawa wote unaowaita wapinzani ni binadamu na wana hisia cha uvumilivu kama binadamu. Ni kwa kiasi gani sisi kama raia tuko tayari kuwajali kwa hali na mali wale tunaodhani ni viongozi? tunaweza kunyoosha vidole kwa hao jamaa, at the same time tukasahau mchango wetu kama wataka mabadiliko.
Ni nani aliyetayari kumpa fedha Baregu baada ya kukosa fedha za chuo, au nani aliyemkumbuka Lamwai baada ya kuporwa vyeti vyake vyote vya kazi? nani anayeweza kuwaza au kufikiri shida wanazozipata hawa viongozi?
watanzania wengi hawapo kwa ajili ya mabadiliko, labda utajiaminisha ukiwa JF! but believe me out there people are like fish they may swim as the water course directs! hamna michango kwa vyama, wala viongozi hawa wanapopata shida.wanapoamua kusema haya narudi CCM basi ''ndio tunaanza kusema mapandikizi''
Kuna mchango mkubwa sana wa raia wenyewe kuwarudisha nyuma hawa wapiganaji!
Kuhusu Zito limejadiliwa sana, na nimekuwa na challenge sana great thinker to see this problem in many dimensions. Zito huyu leo anabebwa na watu jangwani, kesho anaonekana msaliti, ghafla tu!!-siamini!! kutatua tatizo la Zito ndiyo kutatua matatizo ya vyama vyetu.
Tuangalie vyama vinaongozwa vipi, vinafanyaje uchaguzi, uwazi, makundi, na tunaposema chama tunamaanisha chama chenye sifa zote za kuwa chama, na sio chenye sura za kibaguzi wala kutokueleweka katika jamii.
wakati Buchanan unasema la zito, nimekuwa nikitoa challenge kuangalia tatizo la chadema pia, kama source ya haya matatizo ya Zito yanatokana na chadema then we have to find out why, how, and possibly to remedy the problem for future! vyama vingi vimekuwa vikileta matatizo na sisi tumekuwa tukiwalaumu waathirika. na pengine kwa kupenda sana, (na hapa ni tatizo) tumekuwa tunashindwa kusimamia ukweli na kuwa watu wa double standard! challenge yangu ni kuwa , haya yasipodhibitiwa basi aidha hatutakuja kupata mpinzani makini kama akina Tsavangirai au tutaishia hivi hivi, tangu 1992 mpaka leo 2010, still hakuna chama tegemeo la kuitoa CCM madarakani, still unataka kuangalia individual hapa!!
Lingine sijui wewe, huwa namchukulia Zito kama binadamu mwingine, mwenye uhuru wa kutoa maoni yake, na anapotoa maoni hawi rais wa nchi hii, kama wengine wanavyotaka aonekane hivyo. Tatizo la Zito ni kuchallenge idea na kusimamia anachokiamini na hili kwetu wengi ni tatizo!... La kuwa aliye-kinyume chetu ni adui! Juzi juzi sera ya afya ya Obama ilikuwa na ina kuwa challenged hadharani yeye akisikia na kuona yet anajibu vizuri na kutetea hoja zake.
Hayati Nyerere alikuwa mbishi na utakuta Idea na ushauri wa kama akina Mtei hakuuchukua na baadae kuja kugundua was too late. Viongozi wengi leo wa taifa hili ni wabishi miungu watu na ukitaka kugombana nao wewe bishana nao. Hawa viongozi ndio sisi, ndio kioo chetu na mengi wanayoyafanya ndiyo yanaonekana kwa watanzania wengi. JAMANI ANAYEKUJA NA IDEA TOFAUTI SI KUWA NI MBAYA!!
samahani, ila sisi wengi tunatabia ya ubishi, one dimensional thought, sawa kabisa na viongozi wetu, tunachotaka na kuamini kwetu ndiyo sahihi asilimia 100! leo hii tumefika hapa ni kwa sababu hatuna open debate, hakuna watu wa kuchallenge viongozi(zidumu fikra za mwenyekiti), viongozi wanakimbia mijadala na hata kutoa maoni hawapatikani.Katika nyakati ngumu kabisa za watanzania kutaka viongozi wao waseme jambo huwa wako kimya!!! yet we call them leaders
Jamii inayoendelea na iliyokuwa ni ile inayochallenge Idea na si mtu. Zito kwangu mimi sioni ni mtu tishio kabisa, siyo rais, wala PM, sioni woga unatoka wapi wa kutozisikiliza idea zake na kuzichallenge, sorry to say this! issue za Zito zinaonyesha jamii iliyovivu kufikiri, katika watanzania millioni 40, anayesema mambo ni Zito tu? jamani Buchanan haya si matusi kwetu sisi wengine? wewe usiwe mmoja wao!
who is Zito? wengi huwa naona watu wanajidharaulisha, inferiority complex, wengine woga wa kusema, wengine uvivu wa kufikiri, wafuata Mkumbo n.k Mbona hatupati maoni tofauti ya Zito na serikali? yako wapi? nani anasema? mbona hatuyasikii? jamani hapa mimi naona kuna tatizo! Haiwezekani aogopwe mtu asiye rais , PM wala waziri!!! think about it!!
So in long run , kutokana na thread yako na mtazamo wako, tusipojiangalia sisi wananchi na nafasi yetu katika mageuzi, tusipoangalia vyama hivi vinaongozwaje, tusipojiangalia mmoja mmoja, samahani kusema hivi CCM may rule FOREVER, kila siku tutatafuta mchawi
By the way, chart inaonyesha wapinzani wanapata kura chache kadiri miaka inavyoenda mbele! hili hali tuna maendeleo ya teknolojia! tatizo hapa ni Zito na Mrema?
we need to dig deep and see our problem jamani, tusiwabebeshe mzigo wasiostahili, vyama leo vinawaza uchaguzi ili hali kuna mengi ya kurekebisha, wakishindwa --MREMA amesababisha!
watanzania wenzetu kuwapokea kwa mazuria mekundu akina EL, RA, Karamagi n.k still ni matatizo ya akina Mrema!!!
we are not ready to support these opposition leaders at any cost and condition! that is our problem!!
Probably we should wait for an angel!
Believe me uone tulivyoingia kwenye huu mtego wa 'pandikizi, kanunuliwa, n.k'' leo hii kutokana na haya maendeleo mtu yeyote aliye kiongozi yeyote anaweza kuzushiwa kitu, watanzania tumesahau kuna dudu LINAITWA CCM, badala ya kupigana nalo TUNAPIGANA WENYEWE! tunaitana majina, BELIEVE ME kwa miaka 20 ijayo usitegemee kuna kiongozi yeyote wa upinzani atakayekuja kama hao hapo juu! believe me akitokea KAPU NA HATIMA YAKE NI KUITWA 'pandikizi' CCM haoooo....wanapeta
Siamini kabisa kama Mrema ni pandikizi, alikuja kwa walio wake walio wake wamemkataa! wamemwacha frustrated! yet ndani ya CCM mpaka leo ni mmoja wa wenye rkodi nzuri, mtanzania anasema pandikizi.. mnataka ccm leo wasamabaratike watokee akina Mrema, muwaite nao pandikizi
SIFA YA MREMA KWENYE MAGEUZI HAITAFUTIKA KAMWE!!