mkuuwakaya
JF-Expert Member
- Mar 18, 2013
- 1,063
- 1,456
Kwa nyakati tofauti DUCE imetajwa katika masakata mbalimbali ya wanasiasa wanaopitia hapo. Tukianzia na Ludovick Joseph Yule wa movie ya Lwakatare alipitia pale.Siasa zake na ushiriki wake CDM ulikuwa wa mashaka sana na hata kuingia kwenye scandal ya Lwakatare Movie(The Fake Movie). Kama hiyo haitoshi aliyekuwa bosi wa Kitivo cha Elimu DUCE Daktari Kitila Mkumbo naye kafanya madudu ndani ya chama. Ambapo mwishowe kila mwanajamvi anajua kilichomkuta. Sasa hivi tena naye Yona Patrick Mwenyekiti wa CDM Temeke na Laboratory Technician -DUCE amekuja na movie yake FAKE baada ya Kujichubua kwenye paji la uso NA KUJITEKA na kwenda kulala Ununio eti naye katekwa. Hivi wanajamvi kwa scenario ilivyo kuna utekaji wowote pale?Hana mchubuko mikononi , miguuni, wala hakufinywa , wala hakuburuzwa , wala hata kukatwa sehemu yoyote ile zaidi ya Kamchubuko usoni . HUU NI USANII MKUBWA TUULAANI. Huyu jamaa ni nafanya naye kazi ila idara tofauti. Stori zake mara zote katika siasa huwa ni za mashaka. Ile siku kabla hajaenda press conference Lamada November 2013, alisema kwa kinywa chake kuwa yeye kuna siku atakuwa tajiri kupitia siasa zake iwe CCM au CDM. Na alikuwa akionyesha sana kuwa angependa kutumiwa/kupata deal halafu apate kitu kama pesa , hiii ni kwa jinsi nilivyofuatilia maelezo yake. Mtu wa namna hii ni rahisi sana kuwa msaliti. Na hata hii movie yake sasa hivi ni Mwendelezo wa usanii.