Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Nimepta kwenye nyuzi nyingi za wakati huu wa kuelekea uchaguzi na zile za zoezi la kujiandikisha unaona kabis namna Wanasiasa walivyo na uchu na madaraka, wanaonesha jinsi gani kuna fursa huko ndio maana hadi wanataka kutoana roho.
Ila sasa wakitoka hapo utawasikia ooo Siasa hailipi, siasa haina hela, Siasa ni mateso hii nafasi niliyonayo ni utumishi tu il haina hela kama mnavyodhani, vijana jiajirini huku kugumu msije, Eti hii kazi ni ngumu sana, ila anavyoipigania kuipata yuko tayari aue mtu, wanasiasa waongo sana, vijana msije siasa hailipi hailipi mbona nyie mnapigana vikumbo kuipigania nafasi hiyo?
Sisi vijana tukitaka kuja mnasema oo msije hamuwezi huku ni mateso tu kumbe mnatufanya wajinga ili nyie mle mema ya nchi ssi tubaki kuwadekia barabara mpite na viete mlizonunua kwa kodi zetu.
Pia soma: LGE2024 - Kura za Maoni za CCM ngumi zafumuka kila Mahali