Wanasiasa wanavuruga mfumo wa elimu Tanzania

Wanasiasa wanavuruga mfumo wa elimu Tanzania

Tyetyetye

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2014
Posts
1,142
Reaction score
940
Kuna watu wanapata udaktari kwa dakika mbili (udaktari wa heshima) na wale wanaovuja jasho kupata huo udaktari.
Sasa maajabu hao wa dakika mbili wanatukuzwa kwa udaktari huo utadhani bila kutaja Dr fulani wanakuwa kama wamebaki uchi.
Udaktari wa dakika mbili kamwe haupaswi kutajwa mwanzo wa jina ni dhambi. Kwa vile wanafurahia udaktari wa dakika mbili hawawakemei wanaowaita hivyo.
Mfumo wa elimu unavurugwa.
 
Niliandika kwenye comment moja hapa jf kwamba SIASA INATUHARIBIA MFUMO WETU WA ELIMU. Hapa wasomi na wanazuoni wako kimya au wanasubiri uteuzi huku nyuma elimu ambayo ni urithi wa dunia ya sasa ikiendelea kuchezewa.
Sijui lini tutakuwa serious kama taifa. Nina wivu sana na elimu.....natamani nchi nzima ijae wasomi wenye sifa.
 
Upo sahihi kiongozi, kwa Tanzania acha tu wanasiasa watuchezee mpaka pale tutakapokuwa na akili. Maana kwa sasa mambo yapo wazi kabisa, huioni ile tofauti ya msomi na mlamba nyau. Tena kheri kabisa walamba nyau wasomi ndio wamekua hovyo hovyo walamba nyayo za watu
 
Kuna watu wanapata udaktari kwa dakika mbili (udaktari wa heshima) na wale wanaovuja jasho kupata huo udaktari.
Sasa maajabu hao wa dakika mbili wanatukuzwa kwa udaktari huo utadhani bila kutaja Dr fulani wanakuwa kama wamebaki uchi.
Udaktari wa dakika mbili kamwe haupaswi kutajwa mwanzo wa jina ni dhambi. Kwa vile wanafurahia udaktari wa dakika mbili hawawakemei wanaowaita hivyo.
Mfumo wa elimu unavurugwa.
Unamsagia kunguni chief Hangaya siyo?🤣
 
Back
Top Bottom