wanasiasa watch out!!!

wanasiasa watch out!!!

Freetown

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2008
Posts
882
Reaction score
78
Wanasiasa 40 walipata ajali mbaya porini, mkullima mmoja alipoona hivyo alichimba shimo na kuwazika wote kwa pamoja.
Baadaye polisi walikuja na kumhoji kuhusiana na ajali pamoja na maiti na mahojiano yalikuwa hivi:-

Polisi :- Uliona ajali jinsi ilivyotokea?

Mkulima :- Hapana, nilikuta imeshatokea na maiti zimezagaa..

Polisi :- Zipo wapi maiti?

Mkulima :- Nimezizika

Polisi :- Una uhakika wote walikua wamekufa?

Mkulima :- Kuna wengine walikuwa wanalalamika kwamba hawajafa lakini si unajua wanasiasa walivyo waongo, mi nikajua tu wanadanganya nikawazika wote
 
Back
Top Bottom