Wanasimba lialia hamtakiwi kutoa hukumu kwa beki Joash Onyango wakati katika benchi hakuna mbadala wake

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Katika pita pita zangu katika vijiwe vya kahawa vijiwe nongwa pamoja na vijiwe vya vya kidigital vinavyotaka timu ishinde tu hata Kama haina uwezi lakini mashabiki hawalijui Hilo.

Nimepatwa na gadhabu baada yakuona kila shabiki lialia wa simba akirusha mawe kwa beki kitasa joash onyango nakudai kuwa yeye ndiyo tatizo na ndiyo maana tunafungwa eti kwa sababu tu ya penati alizosababisa kwe michezo miwili dhidi ya raja Casablanca.

Nakataa nakupinga lawama zote kumuangushia beki joash onyango, mpira ni mchezo wa wazi, mpira ni mchezo wa makosa yaani "one mistake one goal' that is football.

Nilitazama mechi ya simba vs Casablanca kiukweli hakuna mchezaji aliyeleta matumaini, mtazame shomari kapombe alivyokua akipata tabu dhidi ya mawinga wa Casablanca,
Mtazame mchezaji mahili na tegemezi chama alivyofichwa na viungo wakabaji wa Casablanca.

Tazama viungo wa Kati wa simba namba name na namba sita, je mliyaona makosa yao pale Kati???
Je mliona namna gani inonga alivyokua anavuja dhidi ya mawinga mpaka wanapata nafasi yakumfikia kipa manura ??

Ngoja tutoe hayo magoli mawili ya penati aliyoyasababisa joash onyango Kama msemavyo, yatabaki magoli manne je hayo yote yamefungwa bila ya makosa ya wachezaji ??

Hatupaswi kumtupia lawama onyango, hatakama benchi la ufundi litaamua kumuweka benchi je ni beki gani anayeweza kujituma na kufiti nafasi ya onyango??
Jibu hakuna,

Niwaombe wanasimba lialia mnapotoa lawama kwa mchezaji mmoja mnakosea lakini pia kumbukeni mlimuita nusu mtu, nusu chuma mkimaanisha ni mwamba haswaa.

Ifikie hatua mkubali kuwa kikosi chenu hakina ubora na siyo mzigo wa lawama mnaanza kumtupia mchezaji mmoja utadhani anacheza peke yake.

Nimeandika Kama mdau wa mpira na so shabiki wa mpira NALIA NGWENA
 
Pole sana mkuu

Umekazana mambo ya Simba na yanga.

Nasikitika kuona WATOTO wa Masikini wakibishana 24 hours Simba na yanga.

WATOTO WA MATAJIRI wakipanda ndege kwenda kusoma. Au wakipanda vyeo.

TUENDELEE KUBISHANA
 
Pole sana mkuu

Umekazana mambo ya Simba na yanga.

Nasikitika kuona WATOTO wa Masikini wakibishana 24 hours Simba na yanga.

WATOTO WA MATAJIRI wakipanda ndege kwenda kusoma. Au wakipanda vyeo.

TUENDELEE KUBISHANA
Sasa unataka apande ndege ili akasome wakati umeshasema yeye ni mtoto wa maskini? Acha ujuaji pimbi wewe
 
Pole sana mkuu

Umekazana mambo ya Simba na yanga.

Nasikitika kuona WATOTO wa Masikini wakibishana 24 hours Simba na yanga.

WATOTO WA MATAJIRI wakipanda ndege kwenda kusoma. Au wakipanda vyeo.

TUENDELEE KUBISHANA
Hata wewe nakupa pole sana muda ambao watoto wa matajiri wakipanda ndege kwenda kusoma lakini wew umekazana humu jf kupita kweye kila nyuzi nakukoment upumbavu wako

Bakhresa Hana muda Kama huu wakipumbavu Kama wako,
 
Goli la kwanza ni uzembe wa Inonga lakini jumba bovu anaangushiwa babu Onyango
Siko hapa kumhukumu Onyango ila nataka tu nijue lile goli lakwanza makosa ya Inonga yalikua wapi.

Kwakua nilivyoliona mimi lile goli nikua Inonga alienda kukaba pembeni kwa mtu ambae alikua yuko loose na yule mtu akaupiga kichwa mpira kuudondeshea ndani ya box na kwa bahati mbaya Onyango timing yake haikua sahihi akaukosa ule mpira na jamaa aliekuepo akamalizia.

Shida ya Inonga ilikua wapi!!
 
Kaangalie vizuri clip halafu ndiyo urudi Tena hapa.
 
Unajua kuna tofauti ya kukaba na kuangalia, Inonga alikaba nini pale
 
Tafuta hela



Mabingwa hawahitaji shobo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…